The House of Favourite Newspapers

PENZI LA SUGU LIMEMWACHIA FAIZA UGONJWA MBAYA

 BIPOLAR Disorder ni ugonjwa mbaya wa kisaikolojia. Ni ugonjwa wa kubadilikabadilika kwa hisia. Unahusishwa na mtu kuwa na furaha au huzuni kupita kiasi.

Ni ugonjwa ambao husababisha misimu ya huzuni na furaha iliyopitiliza.

Ni hisia zilizoongezeka ambazo pia hujulikana kama wazimu mkali kutegemea na ukali wake.

Pamoja na dalili nyingine za ugonjwa huu, iliyo kuu ni tabia ya mtu kuwa na furaha au hasira isiyo ya kawaida.

Watu binafsi hujikuta wakifanya uamuzi bila kufikiria vizuri na bila kujali matokeo.

 

Mtu huyu huwa kwenye hatari ya kujitia kitanzi miongoni mwa walio na ugonjwa huu. Pia kuna masuala mengine ya afya ya kiakili kama vile matatizo ya kuwa na wasiwasi na kuwa na matumizi mabaya ya vifaa au dawa ili kuathiri hisia za mtu.

Mara nyingi ugonjwa huu huhusishwa na tatizo la kubadilikabadilika kwa hisia.

Chanzo cha ugonjwa huu kinaweza kisiwe wazi sana, lakini vipengele vya kimazingira na jenetiki huchangia.

Vipengele vya hatari vya kimazingira hujumuisha historia ya unyanyasaji au kupenda kupita kiasi.

Dalili nyingine kwa mtu kama huyu ni pamoja na tatizo la upungufu wa umakini, matatizo ya kiakili yenye kuleta mtazamo, fikra, tabia na mhemko usio wa kawaida.

Matibabu ya ugonjwa huu hujumuisha matibabu ya kisaikolojia sawa na dawa kama vile vidhibiti vya hisia.

Ni tatizo linalosababisha kubadilikabadilika kwa hisia na huathiri takriban 1% ya idadi ya watu ulimwenguni. Weka nukta hapo!

 

FAIZA ALLY

Katika pitapita zangu kwenye vilinge vya habari za mastaa mitandaoni wikiendi iliyopita, nilikutana na mjadala kabambe unaomhusu mwigizaji wa sinema za Kibongo na mjasiriamali, Faiza Ally.

Faiza ni mama wa watoto wawili akiwemo mmoja wa kike aliyezaa na Mbunge wa Mbeya- Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Mbilinyi almaarufu Sugu aitwaye Sasha.

 

Mjadala wa Faiza ulikuja kufuatia waraka wake mrefu kama shuka akieleza namna ambavyo alikuwa ametibuliwa na tukio la Sugu kumvisha pete ya uchumba mwanadada Happiness Masonga.

Sugu alimvisha pete ya uchumba Happy ikiwa ni takriban miaka minne tangu uchumba wake na Faiza ulipoota mbawa.

 

Katika waraka huo, Faiza aliomba uchumba huo uvunjike ili Sugu arudi kwake kisha wafunge ndoa kwani anaamini yeye ndiye mwanaume wa maisha yake yaliyobaki hapa duniani.

Kwa nyakati tofauti, Faiza amekuwa akieleza ni kwa jinsi gani alioza kwa Sugu kutokana na penzi lao lilivyokuwa moto chini. Mara kadhaa hasa Sugu anapokuwa na tukio lolote kubwa, Faiza amekuwa akijitokeza na kueleza hisia zake juu ya mheshimiwa huyo.

Tatizo ambalo Faiza amekuwa nalo ni kubadilikabadilika juu ya hisia zake kwa Sugu. Kuna wakati huwa anamponda kupita kiasi akilalamika kuwa Sugu hamjali mtoto wake huyo ambaye anaishi na Faiza jijini Dar.

Wakati anaachana na Sugu, Faiza alitamka maneno mabaya mno juu ya Sugu akionekana mwenye hasira za kutosha kutokana na kuvunjika kwa penzi lao.

 

Ni kweli kwamba, kwa mwanamke inauma mno anapozalishwa kisha mwanaume kumwachia jukumu la kulea mwenyewe, lakini ni vyema akajua kuchunga mdomo na kuacha kuanika mambo mabaya ya mzazi mwenzake mtandaoni.

Ni dhahiri kwamba, bila kipingamiza, Sugu, kama ilivyokuwa kwa Faiza naye alimpenda mno mwanamama huyo.

Utofauti ni upi? Baada ya wawili hao kuachana, Sugu yeye aliamua kusonga na maisha yake mengine na kukubali kile kilichotokea, lakini Faiza ameshindwa kabisa kusahau na kusonga mbele (to move on).

 

Kwa mujibu wa wataalam wa saikolojia, Faiza amekuwa akisumbuliwa na Bipolar Disorder. Ameshindwa kabisa kuzuia hisia zake na kubadilika mara kwa mara. Kuna wakati anasema anatamani azae mtoto mwingine na Sugu kwa kuwa bado anampenda. Lakini kuna wakati mwingine huibuka na kumponda kwa kuanika siri za penzi lao kutegemeana na alivyoamka.

Wataalam hao wanasema mtu anaweza kudhani Faiza hufanya hivyo kutokana na kutokuwa na akili nzuri, lakini ukweli ni kwamba hujikuta akifanya hivyo kutokana na hisia anazokuwa nazo juu ya mpenzi wake huyo wa zamani.

 

Kinachoonekana, penzi la Sugu limekuwa ni gumu kufutika kichwani mwa Faiza na kujikuta akipambana na gonjwa la Bipolar Disorder.

Kwa mtazamo wangu, Faiza anapaswa kutokuwa mkali kutokana na kile alichokipitia kwa Sugu, badala yake ajitahidi mno kusimamia hisia zake na kukubali kuwa yeye na Sugu mapenzi yalikwisha hivyo asonge mbele na kumwacha mwenzake ambaye alishaamua kusonga mbele!

Makala: Sifael Paul

Comments are closed.