The House of Favourite Newspapers

Programu ya “mpaper” yatajwa kuwania tuzo 2 Afrika

0

m paper

PROGRAMU ya kusomea magazeti kwenye simu za mikononi hapa nchini ya mPaper jana imetajwa kuwania tuzo mbili za ugunduzi kwa mwaka 2015 kutoka shirika la AppsAfrica lililopo nchini Afrika Kusini.

mPaper imetajwa kuwania tuzo mbili, moja ni Programu bora ya Afrika na nyingine ni Tuzo ya ugunduzi bora wa kielimu.

Hizi ni habari njema kwa Watanzania wote, hasa ukizingatia ni wiki hii mwanamuziki wa Kitanzania, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ alitwaa tuzo tatu za kimataifa za AFRIMMA huko Marekani.

mPaper ni programu ya Kitanzania inayokuwezesha kusoma magazeti yote kama yalivyo pamoja na vitabu mbalimbali kwenye simu yako ya mkononi.

mPaper imegunduliwa nchini Tanzania na imetengezwa na kampuni nguli ya matangazo mtandaoni ya SmartCodes.

Baada ya kutajwa kuwania tuzo hizo, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa SmartCodes, Bwana Edwin Bruno alikuwa na haya ya kusema:

“Tumepokea kwa furaha sana uteuzi huu wa kuwania tuzo hizi za kimataifa, kwa niaba ya timu nzima nyuma ya mPaper, natoa shukrani za pekee kwa mtandao wa AppsAfrica kwa kuitambua na kuipa heshima ya kipekee programu hii. Inatia moyo kuona kile unachokifanya kinaonekana ndani na nje ya nchi.”

Kupitia programu hii ya mPaper unaweza kupata magazeti yote ya Global Publishers Ltd ambayo ni Uwazi, Amani, Ijumaa, Championi na Risasi.

Leave A Reply