The House of Favourite Newspapers

Kocha Simba: TFF wanaiangusha Yanga

KOCHA Mkuu wa simba, Mbelgiji, Patrick Aussems amefichua kuwa haoni dalili za timu Tanzania kuweza kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa msimu huu kutokana na ratiba mbovu ya shirikisho la soka Tanzania (Tff) kuingiliana na ya shirikisho la soka Afrika (CAf).

 

Aussems ametoa kauli hiyo akizilenga Simba anayoifundisha na Yanga ambazo zinashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika huku kwa upande wa Shirikisho ikiwa ni Azam FC na KMC.

 

Kocha huyo kwa sasa anashikilia rekodi ya kuifikisha Simba katika Hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita, anaamini nafasi ya timu za Tanzania ikiwemo Simba na Yanga kufanya vizuri katika michuano hiyo ni ndogo tofauti na matarajio ya wengi.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Aussems alisema kuwa kutokana na ratiba ya Ligi Kuu Bara iliyotolewa na TFF, haiwezi kuwa msaada kwa timu za Tanzania kuweza kufanya vizuri katika michuano ya CAF msimu huu. “Nisiwe muongo ratiba ya ligi imekuwa ni ajabu na inashangaza kwa sababu inatoa nafasi finyu kwa wawakilishi wa nchi katika michuano ya kimataifa sasa sioni kama kuna timu itaweza kufika kwenye hatua nzuri.

 

“Angalia mechi zetu za ligi za kwanza na zile za kimataifa, hata kama itakuwa imeondolewa lakini bado itaendelea kuziathiri timu zote za Tanzania ambazo zinashiriki michuano ya Caf kwa sababu ya kuingilia kwa tarehe za mechi, mwisho wa siku tunakwenda kuwatesa wachezaji kama ilivyokuwa msimu uliopita na jambo hili linaumiza sana linaumiza,” alisema Aussems.

STORI NA IBrahim mussa, Dar es salaam

Comments are closed.