The House of Favourite Newspapers

ROSa Ree Siyo Yule ‘Mungu Mwanamke’

MIONGONI mwa mabinti wenye vipaji vikubwa mno wanaofanya muziki huu wa Bongo Fleva katika kipengele cha ‘Keep It Hip Hop’ ni Rosa Ree.

 

Rosa Ree ambaye jina lake halisi ni Rosery Robert, alianza kusikika mwaka 2015 aliposainiwa kwenye Lebo ya The Industry inayomilikiwa na prodyuza Emmanuel Mkono ‘Nahreel’ na Aika Marealle wa Kundi la Navy Kenzo.

 

Akiwa na lebo hiyo, Rosa Ree ambaye ni mzaliwa wa Moshi, Kilimanjaro, alisikika na ngoma kali kama One Time iliyomtambulisha kwenye gemu la Bongo Fleva kisha zikafuata nyingine za Up In The Air, Way Up, Marathon, Dow, Asante Baba U.N.I.T.Y na nyingine kibao.

 

Rosa Ree alianza muziki tangu utotoni na kitu ambacho kipo kwenye damu. Akiwa mtoto alipenda sana kuimba nyimbo za mastaa kama Faith Evans na P Didy kabla ya kujikita kanisani na kubobea kwenye mapambio.

 

Rose Ree aliyezaliwa Aprili 21, 1995, wakati anaanza gemu alijinasibu kama bonge moja la mgumu huku akijiita ‘The Goddess’ yaani ‘Mungu Mwanamke’, lakini kadiri siku zinavyoyoyoma huo ‘u-goddess’ unapotea kidogokidogo hasa baada ya kuondoka kwenye Lebo ya The Industry.

 

Kwa sasa Rosa Ree anaonekana kulegeza ile mikato yake hasa kwenye eneo la ugumu na kuonekana siyo yule wa zamani.

Hata aina ya ngoma na mashairi yake siyo yale magumu yaliyomuweka kwenye kapu moja na wakali wa Hip Hop Bongo kama Fid Q kwenye ngoma waliyoshirikiana ya Korasi. Siku hizi anasikika kwenye ngoma za kawaida kama Ungese na Nguvu za Kiume.

Wiki iliyopita Rosa Ree, kwa mara nyingine aliwashtua mashabiki wake baada ya kusambaa kwa video chafu (dirty version) ya Wimbo wa Vitamin U alioshirikishwa na msanii kutoka nchi jirani ya Kenya, Timmy Tdat, anayesemekana kuwa wana uhusiano wa kimapenzi.

Kupitia Over Ze Weekend, Rosa Ree ambaye mwaka jana picha zake chafu na jamaa huyo pia zilisambaa na kuzua mjadala kila kona, anafunguka tafrani iliyotokea juu ya sakata hilo lililosababisha kuitwa na Bodi ya Filamu Tanzania na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata);

 

OVER ZE WEEKEND: Video chafu ya wimbo wenu imeondolewa kwenye Mtandao wa YouTube na wewe sasa unapata misukosuko. Je, kwa nini mlitoa video hiyo chafu?

 

ROSA REE: Unajua unapokuwa mwanamuziki au msanii unakuwa na mawazo tofauti, lakini humaanishi kumkwaza mtu hata mmoja. Ni namna tu ya kufikisha burudani yako ipasavyo na hicho ndicho kilichotokea kwetu.

 

OVER ZE WEEKEND: Mliwaza nini hadi mkatengeneza na kuachia video chafu kama ile au kuna sehemu mlichukua wazo kama hilo?

 

ROSA REE: Kwanza mashabiki wangu wajue tu kwamba ile video ni ya wimbo ambao mimi nimeshirikishwa tu na siyo yangu. Kingine ni kwamba kwa sababu kuna upungufu umetokea ambao mashabiki wetu hawajapendezwa nao, basi tumetii haraka na huo wimbo hauwezi kusikika au kuonekana tena. Ninawaomba sana mashabiki na wote walioguswa na jambo hili wanisamehe mno!

 

OVER ZE WEEKEND: Lakini si mmetumia gharama kubwa kutengeneza video ya wimbo huo na sasa mme-pata has-ara? Je, mme-pata has-ara kiasi gani?

 

ROSA REE: Kama nilivyo-sema mwanzo, mimi nimeshiri-kishwa na Timmy kwenye ule wi-mbo, lak-ini siyo kwa-mba mz-igo nim-eua-chia, yeye mwe-nyewe au lawama zote nimpe yeye kwa sababu hakuna aliyenishikia bastola na kuniambia kaa hapo urekodiwe ile video.

 

OVER ZE WEEKEND: Mara nyingi umekuwa ukikanusha kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Timmy, lakini kwenye video ile inaonekana wazi ninyi ni wapenzi kwa jinsi alivyokuwa akikushika sehemu nyeti za mwili wako, bado unabisha?

 

ROSA REE: Nafikiri mtu unapokuwa msanii, unaweza kufanya chochote ili kuonesha uhalisia kwa kile unachofanya na ujumbe unaotaka kufikisha kwa jamii na ndiyo maana hata wasanii wa filamu wanapoigiza kama mke na mume inakuwa siyo kweli bali ni sanaa.

 

OVER ZE WEEKEND: Mashabiki wako wengi walipoiona ile video walihisi labda kuna kilevi ulichotumia kama bangi hadi ukafikia hatua ile ya kurekodiwa video chafu, hilo unalizungumziaje?

 

ROSE REE: Unajua siku zote sipendi kuishi kwenye fikira za watu wanaonifikiria sivyo, maana nikisema nimsikilize kila mtu, ninaweza kupata kichaa. Kingine najua watu wengi wanasema tulikaa uchi, lakini wangeona nyuma ya pazia, wasingesema hivyo kabisa kwani haikuwa hivyo wanavyofikiria.

 

OVER ZE WEEKEND: Vipi kuhusu wazazi wako walipoiona ile video nini kimetokea?

ROSA REE: Ndiyo maana nikasema niombe radhi kwa sababu watu wangu hawakupendezwa na hilo wakiwemo wazazi wangu. Sidhani kama mtu anakuwa anapenda hilo litokee.

 

OVER ZE WEEKEND: Vipi kuhusu Bodi ya Filamu Tanzania, wamesemaje?

ROSE REE: Wamenielimisha vitu vingi mpaka sasa najua mipaka yangu ni ipi na nitakuwa balozi mzuri kwa kuwaelimisha wengine.

IMELDA MTEMA

 

Comments are closed.