The House of Favourite Newspapers

TRA Yafafanua Ongezeko Ushuru wa Magari

0

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa ufafanuzi taarifa juu ya kupanda kwa gharama za kodi za magari yaliyotumika yanayoingia nchini.

 

Ufafanuzi huo umekuja wakati kukiwa na malalamiko  ya wafanyabiashara ya magari wakidai kuwepo kwa ongezeko la kodi za magari ya mitumba.

 

TRA imesema, ushuru hutozwa kutokana na umri wa gari ambao hufuata mwaka wa kalenda. Magari madogo yenye umri wa miaka nane hadi tisa hutozwa ushuru wa bidhaa wa 15% na zaidi ya hapo hutozwa 30%.

 

Hivyo ushuru unaonekana kupanda kwa kuwa kuna walioagiza magari yenye miaka tisa mwaka 2020 lakini yameanza kuingia nchini mwaka 2021 hivyo wanalipa ushuru 30%.

 

“Hivyo ikiwa mwingizaji aliagiza gari binafsi lenye umri wa miaka tisa mwaka 2020 na likaingia nchini mwaka 2021 itatozwa ushuru wa bidhaa kwenye umri wa asilimia 30 badala ya asilimia 15 ambayo ingetozwa  ikiwa gari yake ingewasili kabla ya mwaka huu,” imesema TRA.

 

Mamlaka hayo yamefafanua kuwa kutokana na sababu hiyo waingizaji wa magari yenye umri huo walioagiza mwaka 2020 na kuingia mwaka 2021 ni wazi kuwa kodi kwenye gari aliloagiza itaongezeka

Leave A Reply