The House of Favourite Newspapers

Ajali: Escudo Yaiparamia Bajaji

0

Gari aina ya suzuki Escudo imegongana Bajaji katika eneo la CCM kata ya Ilomba Jijini Mbeya majira ya saa mbili asubuhi Aprili, 27/ 2024.

Kwa mujibu wa shuhuda wanasema dereva wa Escudo alikuwa anaingia barabara kuu gari limemshinda kukata kona akaiparamia na kuigonga bajaji ambayo ilikuwa na dereva iliyokuwa ikielekea mjini.

“Huyu wa gari ametoka huku kituo cha Polisi Ilomba sasa wakati anaingia barabara kuu gari limemshinda kukata kona akaiparamia bajaji cha kushukuru Mungu wote wametoa salama wa bajaji hata wa gari maana hawakuwemo abaria kwenye vyombo vyote viwili,” amesema shuhuda.

Leave A Reply