The House of Favourite Newspapers

Serikali yaandaa mkakati kukomesha migogoro ya ardhi

0

1Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Ukuzaji wa Viumbe Majini, Kajitanus Osewe, Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo nchini, Dk. Abdu Hyghaimo na Ofisa Mawasiliano wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Judith Mhina.

2.Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo hapa nchini, Dk.Abdu Hyghaimo (wapili kushoto) akitoa ufafanuzi wa jambo.Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo nchini, Dk. Abdu Hyghaimo (wapili kushoto) akitoa ufafanuzi wa jambo.

3.Wanahabari wakifuatilia mkutano huo. Wanahabari wakifuatilia mkutano huo.

SERIKALI kupitia Wizara ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi, ipo mbioni kuandaa waraka wa matumizi endelevu ya ardhi utakaowezesha kupata suluhu migogoro ya ardhi nchini.
Akizungumza leo na wanahabari jijini Dar es Salaam kuhusu mapigano baina ya wakulima na wafugaji, Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo Tanzania, Dk. Abdu Hayghaimo amesema ni vyema wananchi wakaupokea waraka huo utakapotolewa hivi karibuni kwa kutumia kamati zitakazoundwa kuusimamia kutafuta suluhu ya migogoro hiyo.
Hayghaimo amesema kamati hizo zitaundwa kwa ufanisi wa hali ya juu kuzingatia taratibu, kanuni na sheria husika na uwakilishi wa pande zote mbili za wakulima na wafugaji ili kuwezesha kusaidia kwa kiwango kikubwa kuondoa migogoro inayoendelea kutokea nchini.
Aidha, amesema jamii inatakiwa kujiwekea utaratibu wa kufuata sheria na ngazi za maamuzi badala ya kujichukulia sheria mikononi ambazo huleta madhara makubwa miongoni mwa jamii.
Amesema kuwa kwa mujibu wa sheria ya Ustawi wa Wanyama ya mwaka 2008, sura 154 kifungu cha 4 kinachoelezea haki zote za wanyama ni pamoja na kulindwa dhidi ya maumivu yoyote, magonjwa na mateso na hata kuwasababishia vifo, huku akisema kifungu cha 49 hadi 58 kinaonesha taratibu za kufuatwa endapo mnyama anakutwa katika eneo lisilo rasmi.
Kwa upande mwingine Hayghaimo alieleza kitendo kilichofanyika kwa wanyama kuuawa kwenye Kijiji cha Dihimba, Wilayani Mvomero ni kosa kisheria hivyo serikali itahakikisha wahusika waliofanya vitendo hivyo wanashughulikiwa ipasavyo. Mapigano hayo yaliyotokea Desemba 11, mwaka huu Mkoa wa Morogoro na kudumu kwa takribani siku tatu ambapo yalisababisha vifo na kujeruhiwa kwa ng’ombe na watu.
Kwenye tukio hilo, mkulima mmoja alifariki dunia, wengine wanne walijeruhiwa huku kukitokea vifo 79 vya ng’ombe na wengine 72 kujeruhiwa vibaya.
NA DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply