The House of Favourite Newspapers
gunners X

Rais Mwinyi Atangaza Mawaziri Wateule Wa Serikali Ya Mapinduzi Ya Zanzibar -Video

0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametangaza uteuzi wa Mawaziri na Naibu Mawaziri wateule, hatua inayolenga kuimarisha kasi ya maendeleo katika kipindi cha pili cha Awamu ya Nane ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Akizungumza leo, tarehe 13 Novemba 2025, Ikulu Zanzibar, Rais Dkt. Mwinyi amesema Serikali katika awamu hii itakuwa na wizara 20 badala ya 18 zilizokuwepo awali, ili kuongeza ufanisi wa utendaji Serikalini.

Katika uteuzi huo, Rais Dkt. Mwinyi amesisitiza weledi, uadilifu na uzingatiaji wa maslahi mapana ya Taifa, sambamba na kutoa huduma kwa wananchi kwa uwazi na ufanisi.

Ameeleza kuwa uteuzi huo umezingatia uwiano wa kijinsia, uwakilishi wa Unguja na Pemba, pamoja na uzoefu wa viongozi katika sekta zao husika.

Halikadhalika, Rais Dkt. Mwinyi amesema kuwa nafasi za Wizara nne zikiwemo Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Afya, Utalii na Mambo ya Kale, pamoja na Biashara na Maendeleo ya Viwanda , zitaachwa wazi kwa muda hadi Serikali ikamilishe makubaliano na Chama cha ACT Wazalendo katika kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Mawaziri wateule hao wanatarajiwa kuapishwa Jumamosi tarehe 15 Novemba 2025 kuanzia saa 8:00 mchana, Ikulu Zanzibar.

Leave A Reply