The House of Favourite Newspapers
gunners X

Singida Black Stars Yafanya Mabadiliko Makuu: Ouma Kocha Mkuu, Najjar Meneja Mkuu

0
Miguel Angel Gamondi

Singida Black Stars imethibitisha kumteua David Ouma kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo, akichukua nafasi ya Miguel Angel Gamondi, ambaye sasa ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa klabu.

Taarifa rasmi iliyotolewa leo Januari 5, 2025, imeeleza kuwa Ouma, ambaye awali alikuwa kocha msaidizi, atashirikiana na makocha wasaidizi Mousa Nd’aw na Muhibu Kanu.

Aidha, klabu hiyo imemteua Othmen Najjar kuwa Meneja Mkuu wa timu huku Ramadhani Nsanzurwimo, aliyekuwa Mkurugenzi wa Ufundi, akibadilishwa kuwa Mshauri wa Ufundi.

Singida Black Stars pia imesema haikuwapo na pingamizi lolote kwa Kocha Gamondi kuteuliwa kuwa kocha mkuu wa kudumu wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), endapo mamlaka husika yataona inafaa.

Leave A Reply