The House of Favourite Newspapers

Basata Yazindua Matukio ya Siku ya Msanii 2016

0

BASATA (1)

Mshereheshaji katika hafla hiyo, Chris Mauki.

BASATA (2)

 Mgeni rasmi ambaye ni Katibu wa Wizara ya  Habari,  Utamadunim  Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabrel akisikiliza jambo.

BASATA (3)

Mgeni rasmi akisikiliza jambo kwa Katibu Mtendaji wa Basata (wa tatu kushoto), Godfrey Mngereza walipokuwa wakitazama ngoma iliyokuwa ikitumbuiza.

BASATA (4)

Wasanii wa filamu Mzee Chilo na mwenzake mama Mgata katika pozi.

BASATA (5)

Wasanii katika pozi.  

Na Hamida Hassan
SHEREHE za uzinduzi wa Siku ya Msanii 2016 zilizinduliwa rasmi jana kwenye ukumbi wa Alliance Francoise ambapo wasanii wa kazi mbalimbali walihudhuria. Siku ya Msanii 2016 inatarajiwa kufanyika Oktoba 29 mwaka huu.

Katika uzinduzi huo ulioandaliwa na Baraza la Sanaa la Taifa  ‘Basata’ chini ya Katibu Mtendaji Godfrey L. Mngereza, mgeni rasmi alitarajiwa kuwa Waziri wa  Habari,  Utamaduni , Sanaa na Michezo Mhe. Moses Nape Nauye ambaye aliwakilishwa na Katibu wa wizara yake, Prof. Elisante Ole Gabriel.

Hafla hiyo fupi ilieleza mipango ya mwaka huu ikiwa ni pamoja na kutangaza kauli mbiu ya mwaka huu  ambayo ni ‘Nguvu ya Sanaa’ ikijumuisha sanaa ya ufundi, muziki, maonesho na filamu kwa ujumla.

Baadhi ya wasanii waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Mzee Chilo, Mama Mjata, Mrisho Mpoto, Stara Thomas na wengine wengi wakiwemo wasanii wa maonesho na ufundi.

Katika siku ya msanii zimeandaliwa tuzo tano ambazo zitatolewa siku ya maadhimisho hayo na ili kuleta tija maonesho ya mara kwa mara yatafanyika mpaka siku ya kilele cha maadhimisho ikiwa ni pamoja na mafunzo kwa watoto wa shule za msingi,  kutakuwa na kongamano la sanaa, maonesho ya kazi mbalimbali za sanaa na shughuli za kisanaa kwa ujumla.

Leave A Reply