The House of Favourite Newspapers

ABDUL NONDO AFUNGUKA WANAFUNZI BUNGANDO KUTIMULIWA – VIDEO

Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TNSP), Abdul Nondo ameiomba serikali kupitia mamlaka zake, kuhakikisha zinafuatilia kwa kina sakata la wanafunzi wa Chuo Kikuu Katoliki cha Afya na Sayansi Shirikishi (CUHAS) -Bugando cha jijini Mwanza kusimamishwa masomo na kufukuzwa chuoni kwa baadhi ya wanafunzi chuo hicho.

 

Nondo amesema kwamba wanafunzi 10 wa Chuo cha Bugando, akiwemo aliyekuwa Rais wa Serikali ya Wanafunzi, Timon Stephen na aliyekuwa Spika wa Bunge la Wanafunzi, Godfrey Lameck wamesimamishwa masomo kutokana na msuguano uliokuwepo kati yao na uongozi wa chuo.

 

Aidha, Nondo ameiomba serikali kufuatilia kwa kina sakata la wanafunzi hao kusimamishwa na wengine kufukuzwa kabisa chuoni hapo kwani walikuwa wakitetea haki za msingi za wanafunzi wenzao, ambazo zilikuwa zikivunjwa na uongozi wa chuo hicho.

MSIKIE NONDO AKIFUNGUKA

Comments are closed.