The House of Favourite Newspapers

Airtel, SportPesa wawazawadia washindi wa AMSHA AMSHA USHINDE NA AIRTEL MONEY

Meneja Uhusiano wa SportPesa Tanzania, Sabrina Msuya (kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Washindi hao kutoka kushoto ni Venus Malima,Kiliani Moyo, na Frank Mbwana ambao wameshinda simu za kisasa  smartphone Samsung galaxy.
Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando (kushoto) na mmoja ya washindi wa promosheni ya AMSHA AMSHA USHINDE NA AIRTEL MONEY Frank Mbwana wakiangalia simu ya smartphone ambayo ni moja ya zawadi. 
Mmoja wa washindi hao akionyesha simu ya awali aliyokuwa akiitumia kabla ya kukabidhiwa simu ya smartphone.

 

Kampuni ya simu ya  Airtel  Tanzania kwa kushirikiana na kampuni ya kubashiri ya SportPesa imewazaidia washindi watatu wa promosheni ya  wa Amsha Amsha ushinde na Airtel Money.

 

Washindi hao ni Kiliani Moyo, Venus Malima na Frank Mbwana ambao wameshinda simu za kisasa  smartphone Samsung galaxy.

 

Washindi hao wameshinda katika droo ya kwanza ya promosheni hiyo ambapo jumla washindi  21 walipatikana.

 

 

Mbali ya washindi wa simu ya mkononi, pia kulikuwa na mshindi wa  televisheni ambaye ni Mkulima wa Tabora, Charles Peter ambaye pia alizawadiwa king’amuzi cha  Star Times.

 

Washindi wengine ni HiIlary Ngarweze, Grace Nsasi, Juma Juma, Chriphod Bunyinyiga, Venus Lugela, Haji Haruna, Jaffari  Nkomee na Sige Fadhil.

 

Walioshinda jezi ni Faraji Namwanga, Omary Said Kaombe, Moses Lifunga, Maulid Salum, Omary Kirangio, Beno Milinga, Augustine Kasiasto, Elias Mgarula na Karato Joel.

 

Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando alisema kuwa bado wana zawadi nyingi ambazo zitatolewa kwa washindi na kuwaomba watu waendelee kucheza ili kushinda.

 

“Kuna walikuwa hawaamini kuwa kuna zawadi hizi, sasa kwa kuwapa zawadi hawa washindi watatu ni njia pekee ya kuwahakikishia wateja wetu kuwa zoezi limeanza rasmi na kuna nafasi kubwa ya kushinda,” alisema Mmbando.

 

Meneja Uhusiano wa SportPesa Tanzania, Sabrina Msuya aliwaomba Watanzania kutumia fursa ya promosheni hiyo na kucheza mchezo wa kubahatisha na kampuni yao ili washinde zawadi nono.

 

Sabrina  alisema kuwa  kutumia kampuni yao na Airtel, watanzania wanafursa kubwa ya kujishindia zawadi hizo ambazo zinaweza kubadili maisha yao.

Comments are closed.