The House of Favourite Newspapers

Airtel yazindua huduma ya kutuma fedha nje ya nchi

Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando (kulia) akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kutangaza huduma za kutuma na kupokea fedha kutoka Airtel Kenya kwa kutumia huduma ya Airtel Money kwa gharama ile ile. Huduma hii inalenga kurahisha ukuaji wa biashara baina ya nchi hizi mbili. Kushoto ni Meneja Airtel Money Airtel Tanzania Fidelis Mwebese.
Meneja Airtel Money Airtel Tanzania Fidelis Mwebese (kushoto) akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kutangaza huduma za kutuma na kupokea fedha kutoka Airtel Kenya kwa kutumia huduma ya Airtel Money kwa gharama ile ile.
Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando (kulia) na Meneja Airtel Money Airtel Tanzania Fidelis Mwebese (kushoto) wakionyesha bango baada ya kuzindua huduma ya za kutuma na kupokea fedha kutoka Airtel Kenya kwa kutumia huduma ya Airtel Money.

 

Kampuni ya simu za mkononi Airtel Tanzania imeendelea kuimarisha huduma zake za Airtel Money ambapo kwa sasa mteja anaweza akatuma na kupokea fedha kutoka Kenya kupitia Airtel Money ikiwa ni moja ya jitahada za kukuza huduma za kifedha na kuimarisha biashara baina ya nchi hizi mbili.

 

 

Hatua imekuja baada ya Airtel Tanzania kuungana na wenzao Airtel Kenya kuzindua huduma hii ya kutuma fedha kwa kupitia simu za mkononi ambapo wateja zaidi ya milioni 8 wataweza kufaidika na huduma hiyo.

 

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kutangaza huduma hiyo Meneja Uhusiano Airtel Tanzania, Jackson Mmbando alisema, “Kwa mara nyingine huduma ya Airtel Money inaendelea kupanuka na  kuwafikia wateja wengi kwa kuwawezesha kutuma na kupokea fedha kutoka nje ya nchi. Uzinduzi huu wa kutuma fedha kati ya Tanzania na Kenya kwa kupitia simu za mkononi yaani Airtel Money ni rahisi na haraka na utakuwa wakipee kwa hapa nchini kwetu’.

 

Ili mteja aweze kutuma Pesa kwa Kenya kwa mteja yoyote wa Airtel atatakiwa kufuata hatua hizi.

  1. Piga *150*60# Ili kufikia Kwenye Menyu ya Airtel Money
  1. Chagua 1: Tuma pesa
  1. Chagua 5: Tuma Pesa Nje ya Nchi
  1. Chagua 1. Airtel Kenya
  1. Weka Namba ya Mpokeaji  ( Awe mtumiaji wa Airtel Kenya )
  1. Weka Kiasi unachotuma (katika Tshs.)
  1. Chagua Sababu ya Kutuma Pesa kenya
  1. Weka Namba yako ya Siri ya Airtel Money, Alisema Mmbando.

 

 

Mmbando aliongeza ‘Airtel Money inazidi kuwa imara na kuvutia watumiaji wengi kutokana na kuwa na huduma za haraka, za uhakika na salama. Huduma hii ya kutuma fedha kwenda nje ya nchi kwa kutumia simu za mkononi ni rahisi kwa kulinganisha na njia nyingine za kawaida  zilizokuwepo awali, alisema Mmbando, huku akiongeza kuwa mteja wa Airtel Money kutoka Kenya atapokea fedha zake papo hapo baada ya kuwa tu muamala umekamilika.

 

Kwa upande wake, Meneja wa Airtel Money Bw, Fidelis Mwebesa alisema kuwa kulingana na tafiti za Benki ya Dunia ya mwaka 2018, zaidi ya miamala yenye thamani ya Tzs 5.3 trilioni ilitumwa kutoka Tanzania kwenda Kenya kwa mwaka huo. Hata hivyo, taarifa zaidi zinaeleza kuwa kiwango hiki ni kidogo kwani kuna watu wengi ambao hutumia njia hatarashi za kutuma fedha kama vile kutumia  marafiki wanoasafiri kwa mabasi au njia tofauti na hizo”.

 

 

Airtel Money inazindua huduma hiyo leo ikiwa tayari inatoa huduma za kifedha kwa mtandao kwa wateja wake nchini kwa kushirikiano na nchi nyingine  ambapo Airtel inafanya Biashara kwa kuwawezesha wateja wake kupokea pesa kupitia Airtel Money toka nchi  kama Zambia, Malawi na pia simu zao za mkononi kwenye mataifa mengine kama Qatar, Oman, Afrika Kusini, Uingereza, Shelisheli na Falme za Kiarabu.

Comments are closed.