The House of Favourite Newspapers

Ajali ya Basi la Mohammed Trans Yaua Watatu Manyoni, Singida

mohammed-transTAARIFA zilizotufikia hivi punde, zinaeleza kuwa basi la Kampuni ya Mohammed Trans limepata ajali mapema leo na kuua watu 3 huku wengine 6 wakijeruhiwa nje kidogo ya Mji wa Manyoni mkoani Singida.

Aidha, inasemekana kuwa basi hilo lilikuwa limekodiwa na walimu ambao walikuwa wakisafiri kutoka jijini Tanga.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, chanzo cha ajali hiyo ni gari dogo lililokuwa limeegeshwa barabarani bila tahadhari yoyote, mbele ya basi kulikuwa kuna lori la mafuta hivyo dereva wa lori alipoona mbele kuna gari limepaki na yeye akatanua kwa haraka.

Wakati huohuo, basi nalo lilikuwa linataka ku-overtake hivyo dereva wa basi akashindwa kulimudu kutokana na mwendokasi hivyo kuligonga lori la mafuta kwa nyuma na kutoboka kitu kilichosababisha kumwagika mafuta barabarani licha ya kwamba hayakushika moto.

Comments are closed.