The House of Favourite Newspapers

Ajali ya Ndanda Yaahirisha Michezo Miwili

KUFUATIA ajali Waliyopata timu ya Ndanda walipokuwa safarini kuelekea katika mchezo wa ligi dhidi ya Kagera, Bodi ya Ligi imeipa timu hiyo mapumziko huku michezo yao miwili waliyotakiwa wacheze hivi karibuni, ikisogezwa mbele.

 

Ndanda walitakiwa wacheze mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar Marco Mzumbe, Dar es Salaam jana Oktoba 27 na mwingine walitakiwa kucheza Jumatano ya wiki hii Oktoba 30, ambayo yote imesogezwa mbele.

 

Aidha kufuatia ajali hiyo iliyotokea Nzega Tabora, wachezaji waliopata majeraha ni Aziz Sibo, Hussein Javu, Hemid Koja na Paul Maoja.

 

Hata hivyo, daktari wa timu hiyo Ismail Makumbuli amesema kuwa tayari timu hiyo imewasili jijini Dar katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya vipimo zaidi kwa wachezaji waliopata majeraha kabla ya kurejea mkoani Mtwara.

 

Comments are closed.