The House of Favourite Newspapers

Ajib, Chirwa ‘Waichinja’ Stand Utd, Yanga Yaifikia Simba

KLABU ya Yanga imeichapa Stand United ya mjini Shinyanga kwa bao 3-1 katika mchezo wa ligi Kuu Tanzania bara uliopigwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar leo Machi 12, 2017.

 

Wafungaji kwa upande wa Yanga ni Ally Ally dakika ya 7, Ibrahim Ajib dakika ya 12, Obrey Chirwa dakika ya 85 na upande wa Stand United aliyewafungia bao la kufutia machozi ni Vitalis Mayanga dakika 83.

 

Kwa matokeo hayo Yanga wamepaa na kuifikia nafasi ya pili wakiwa na pointi 46 sawa na Simba SC vinara wa Ligi hiyo wenye pointi 46 pia lakini wakiwa mbele kwa tofautio ya mabao 11 huku akiwa na mchezo mmoja mkononi.

 

Azam wameshushwa hadi nafasi ya tatu wakiwa na pointi 44 huku wakiwa na mchezo mmoja zaidi ya Yanga na miwili zaidi ya Simba.

Comments are closed.