The House of Favourite Newspapers

Ajibu aivutia kasi Lipuli

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu amesema kuwa ameanza mazoezi kwa ajili ya kujiaandaa na mchezo wao dhidi ya Lipuli FC utakaochezwa Uwanja wa Taifa, Dar kesho Jumanne.

 

Yanga ilimkosa kiungo huyo katika mchezo wao dhidi ya KMC ya Kinondoni kutokana na kusumbuliwa na mamivu ya mgongo aliyoyapata katika mchezo wa Yanga dhidi ya Alli­ance FC ambapo walishinda kwa mabao 3-0.

 

“Nipo vizuri kwa sasa nam­shukuru Mungu, ushindani ndani ya ligi ni mkubwa, hilo ni jambo ambalo lipo wazi kwa kuwa kila timu imejipanga kupata matokeo ila tutapambana kuhakikisha tunachukua pointi muhimu.

 

“Ushirikiano uliopo ndani ya kikosi ni mkubwa, mwalimu ana­zidi kutupa maelekezo hali am­bayo inatufanya tuendelee kuwa na mwendelezo mzuri, mashabiki waendelee kutupa sapoti katika kutafuta ushindi,” alisema.

 

Ajibu ndiye mchezaji anayeon­goza kwa kutoa asisti Yanga na Ligi Kuu Bara ambapo mpaka sasa amefikisha nane na ku­funga mabao matatu kati ya 15 waliyonayo, katika michezo nane waliyocheza wakiwa wamejiku­sanyia pointi 22.

Lunyamadzo Mlyuka, Dar es Salaam.

OKWI Alivyokabidhiwa Mpira Baada ya Kupiga Hat Trick

Comments are closed.