Albamu Mpya ya Harmonize Inapikwa
MSANII wa muziki wa Bongo Fleva na CEO wa Lebo ya Konde Gang, Harmonize, amedokeza ujio wa albam yake ya pili ambayo ataipa jina la HIGH SCHOOL.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Harmonize ame-share post ikimwonyesha yupo anaandaa muziki na kuandika HIGH SCHOOL THE Album.
Mapema mwaka huu Harmonize aliachia albam yake ya kwanza iliyoenda kwa jina la AFROEAST ambayo alifanya collabo na wasanii tofauti wakiwemo Burna Boy kutoka Nigeria.
Endapo ataiachia mapema mwaka huu Harmonize atakuwa msanii wa kwanza Tanzania kuachia albam mbili ndani ya mwaka mmoja.
Mbali na hilo mmoja wa mameneja wake anayejulikana kwa jina la Mchopa alifanyiwa mahojiano na Clouds FM na kuthibitisha ujio wa albam hiyo ya pili kwa msanii huyo.
 
			


