The House of Favourite Newspapers

ALICHOSEMA LUKAMBA BAADA YA KUPEWA GARI NA DIAMOND

Msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz akimpongeza Lukamba.

MSANII wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, jana amemzawadia mpiga picha na mwongozaji wa video za Wasafi, Lukamba, gari mpya aina ya Toyota, Alteeza.

 

“Lukamba anakaa Bunju, kuna kipindi alikabwa na kuchukuliwa hadi laptop sasa leo nampatia gari,” aliyasema Diamond Platnumz akiwa  katika tafrija aliy­oifanya mitaa ya Tandale Sokoni katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ambapo aligawa misaada mbalimbali kwa wananchi wa Tandale.

 

Leo kupitia katika page yake ya Instagram Lukamba ameandika: “Hadi Sasa Nimekosa Maneno Ya Kuandika Yatakayoweza Kubeba Hisia Zangu Za Furaha Niliyonayo,Nimekuwa Nikiandika Na Kufuta Kila Neno Ninaloandika Naona Halijitoshelezi Nahisi Halina Uzito Kuelezea Kilichopo Moyoni Mwangu….. Bro @diamondplatnumz umekuwa msaada sana kwa Sisi vijana maskini wenzako, Mungu azidi kukupa moyo wa kidogo unachopata kugawana na wenzako, pia nishkuru uongozi wa @wcb_wasafi kwa kudhamini kidogo changu hii imenipa moyo sana wa kuzidi kujituma zaidi na zaidi
God bless you simbaaa 🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏 @diamondplatnumz

 

Comments are closed.