ALIYEFANYA KAZI NA MAITI MIAKA 32 AFUNGUKA MAZITO

BASIL ENATU (57) ambaye ni mhudumu wa chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Soroti chini Uganda, amesema kuwa anafurahi sana kufanya kazi na maiti kwa takribani miaka 32.

 

Akiongea na gazeti la Daily Monitor, mzee Enatu anasema huwa ni raha sana kufanya kazi na maiti kwani hawasumbui na wamekuwa marafiki wakubwa kwake.

 

“Napenda kufanya kazi na waliofariki kwani maiti hawasumbui kabisa tofauti na watu walio hai”, amesema.

 

Ajira yake ni kuwaosha na kuwavisha maiti na wakati mwingine madaktari pia humtaka awasaidie kuvikata vipande vya mwili wakati wa upasuaji wakati mwili unafanyiwa uchunguzi.

 

Mzee huyo,  baba wa watoto kumi na wawili,  licha kuipenda kazi yake amesema ina changamoto kwani wengi hukataa hata kumsalimia wakihofia mikono yake.


Loading...

Toa comment