The House of Favourite Newspapers

Aliyekuwa Mkurugenzi Wa Jiji Arusha Ahukumiwa Kifungo Cha Miaka 20 Jela – Video

0



Aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Dk. John Pima na wenzake wawili, wamehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela, hukumu iliyotolewa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha baada ya kukutwa na hatia katika makosa ya uhujumu uchumi.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Seraphin Nsana amesema mahakama imewakuta na hatia ya makosa tisa katika kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa ikimkabili Dk. Pima na wenzake.

Licha ya hukumu hiyo, bado Dk. Pima na wenzake wanakabiliwa na kesi nyingine mbali na kesi hio ya Uhujumu Uchumi namba tano ya mwaka 2022.

RAIS SAMIA AMSAIDIA HAITHAM KIM -HARMONIZE ATHIBITISHA KUPITIA MWANA-FA, SIMU MOJA TU AOMBA AMSAIDIE

Leave A Reply