The House of Favourite Newspapers

Mganga Ahukumiwa Miaka 7 Jela Kwa Kumuua Mke Wa Mwanajeshi – Video

0

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Morogoro, imemhukumu kifungo cha miaka 7 jela mkazi wa Kisaki ambaye ni mganga wa kienyeji, Jumanne Peter (28), baada ya kukutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia mteja wake, Christina John mkazi wa Mafisa, Manispaa ya Morogoro.

Akisoma shauri la mauaji katika kesi namba 9 ya mwaka 2023, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Morogoro, Messe Chaba amesema kuwa tukio hilo lilitokea Mei 24, 2020 ambapo mtuhumiwa Jumanne alienda nyumbani kwa marehemu Christina kwa lengo la kumtibu lakini baada ya siku kadhaa, yeye na marehemu walitokomea kusikojulikana.

Ndugu wa marehemu walitoa taarifa kituo cha polisi juu ya kutoonekana kwa ndugu yao, lakini baada ya siku kadhaa, mtuhumiwa Jumanne alikamatwa katika Stendi ya Tabora akiwa na nguo za kijeshi ambazo ni za mume wa marehemu ambaye ni mwanajeshi.

Wakati wa upelelezi, mtuhumiwa Jumanne alikiri kosa kisha kuwapeleka askari mahali alipoufukia mwili wa marehemu.

Baada ya vipimo vya daktari, ilibainika kuwa Christina aliuawa kwa kunyongwa shingoni. Upande wa jamhuri umetoa vielelezo vinne ambavyo vyote vimemtia hatiani Jumanne kwa kuua bila kukusudia.

Leave A Reply