The House of Favourite Newspapers

AMBER LULU AFUNGUKA KURUDI KWA PREZZO

Image result for amber lulu na prezzo

IN love again! Sexy lady wa Bongo Fleva anayefanya poa na ngoma yake ya Jini Kisirani’, Lulu Euggen ‘Amber Lulu’ amefunguka sababu za kurudisha penzi kwa mwanamuziki wa nchini Kenya, Jackson Makini ‘Prezzo’ baada ya kumwagana naye miezi kadhaa iliyopita.

Katika intavyu na Over Ze Weekend, Amber Lulu aliweka wazi kuwa, huko nyuma aliteswa, kuumizwa na mara nyingine kuchezea vitasa kutokana na mapenzi, lakini alipoingia kwa Prezzo alijiona yuko peponi hivyo walipoachana, aliona kuna sababu ya kurudisha mapenzi kwake.

“Nilipata maumivu sana kwenye mapenzi, nilidhalilishwa na kuumizwa. Kuna wakati nilipigwa sana, yaani nilikuwa kama teja, lakini siyo wa kuvuta unga, bali ni wa mapenzi, lakini kwa Prezzo nilikuta tofauti. Nimeona nirudishe penzi kwa nguvu zote,” alisema Amber Lulu ambaye aliwahi kutoka kimapenzi na msanii David Genzi ‘Young D’.

STORI: IMELDA MTEMA, DAR

Comments are closed.