The House of Favourite Newspapers

Amber Lulu, Mume wa Mtu Waangusha Pati

 

 

STORI: WAANDISHI WETU | RISASI MCHANGANYIKO | DAR ES SALAAM

DAR ES SALAAM: Msanii na Video Queen, Amber Lulu anayetamba na Wimbo wa Watakoma, hivi karibuni akiwa na kijana anayedaiwa kuwa mume wa mtu, Joseph Kaburu waliangusha bonge la pati nyumbani kwa jamaa huyo, Bunju B, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Amber ambaye pia ni msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Machi 19, mwaka huu alikuwa anasherehekea siku yake ya kuzaliwa na habari zinasema wawili hao waliamua kuunganisha  pati, kwani mume huyo wa mtu, ambaye anadaiwa kuwa ni mdau wa muziki anayemiliki Kaburu Record ya Sinza naye alikuwa akisherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.


Risasi Mchanganyiko liliibuka ndani ya nyumba ya tukio na kushuhudia waalikwa wakipata vyakula na vinywaji vya nguvu, huku majirani, watayarishaji wa muziki, wasanii na wadau mbalimbali nao wakitimba kwenye pati hiyo.

“Kama ni vinjwaji tumekunywa kwa kweli, ni pati ya kipekee sana, kuhusu nyama choma, ndiyo usiseme kila mtu alikula na kubeba, Kaburu na Amber waliandaa kitu kizuri sana,” alisema mmoja wa wadau.

Amber Lulu hakuweza kupatika na kwenye shughuli hiyo kutokana na ‘kubanwa’ hivyo kushindwa kuz u n g umz i a suala hilo la mume wa mtu, lakini kesho yake, alipatikana kupitia simu yake ya mkononi na kukiri kuwa ni kweli alifanyiwa pati na Kaburu.

Alipotakiwa kueleza ni nani wake, msanii huyo aliomba aachwe kidogo kwani alikuwa anafanya kazi f’lani na kuahidi angepiga baadaye, lakini hadi gazeti hili linakwenda mitamboni hakuweza kupatikana.

Kwa upande wake, Kaburu naye simu yake iliita kwa muda mwingi pasipo kupokelewa.

Baadhi ya mastaa waliohudhuria sherehe hiyo ni pamoja na Mesen Selekta, Nuh Mziwanda, Ice Boy, Mr .T. Touch na wengineo kibao huku MC maarufu Bongo, Zipompapomba akiendesha shughuli kwa ufanisi mkubwa.

ILIKUPITA HII YA AMBER LULU?

 

Comments are closed.