The House of Favourite Newspapers

Amber Rutty, Mpenzi Wake, Wakosa Wadhamini, Warudishwa Rumande

VIDEO vixen wa Bongo, Nascat Abubakary maarufu kwa jina la Amber Rutty na mpenzi wake, Said Bakari Mtopari,  wanaoshtakiwa kwa makosa mawili likiwemo la kufanya mapenzi kinyume na maumbile wanaendelea kusota rumande kwa kukosa wadhamini.
Kesi hiyo iliyokuwa ikiendelea leo Jumatatu, Novemba 12, 2018 Katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam, hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, Agustino Lwizile amewaomba wadhamini wa watuhumiwa hao wajitokeze kwa ajili ya kuwawekea dhamana lakini wakakosekana.
Kesi hiyo ya Amber Rutty na watuhumiwa wenzake wamefika mahakamani hapo kwa ajili ya kusikiliza kesi yao ambayo ilikuwa imekuja kwa ajili ya kutajwa ambapo baada ya kukosekana kwa wadhamini, wahuhumiwa hao wamerudishwa rumande na kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 26 mwaka huu ambapo itarudi kwa ajili ya kutajwa.

MAGUFULI AMWAPISHA WAITARA, MAWAZIRI WAPYA IKULU

Comments are closed.