Amnyoa Kipara Mkewe Alipokuta Nywele Kwenye Chakula

BABLU MONDAL mwenye umri wa miaka 35 mkazi wa Joypurhat, nchini India, amemnyoa mkewe upara baada ya kukuta nywele kwenye wali na maziwa alivyoandaliwa na mkewe.

 

Mwanaume huyo amefanya kitendo hicho bila ya ridhaa ya mkewe,  hali iliyowalazimisha wakazi wa eneo la Joypurhat kupiga simu polisi kuwajulisha, ambapo walifika na kumkamata Bablu kwa tuhuma za kukiuka #HakiZaBinadamu#  kwani mkewe alikuwa na haki ya kuridhia kunyoa nywele zake au kukataa.

 

Wanaharakati wamepiga kelele kuhusu tukio hilo wakisema huo ni ukiukwaji wa haki za wanawake.


Loading...

Toa comment