The House of Favourite Newspapers

Anyongwa Hadi Kufa Baada ya Kumchoma Mkewe na Kurusha Video Tik Tik

0

Tang Lu; ni raia wa nchini China ambaye amenyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia katika kesi iliyokuwa ikimkabili ya kumchoma mke wake moto hadi kufa huku akimrekodi video na kuirusha live kupitia Mtandao wa TikTok.

 

Tang Lu alimchoma moto mke wake wa zamani Septemba 2020 huku akirekodi moja kwa moja tukio hilo la kikatili, jambo lililosababisha mwanamke huyo aliyekuwa na umri wa miaka 30 kufariki dunia kutokana na majeraha aliyoyapata.

 

Mahakama nchini humo imetoa taarifa yake fupi kwamba imetekeleza hukumu hiyo ya kifo cha Tang Lu japokuwa Tang alikuwa amekata rufaa dhidi ya hukumu yake ya kifo, lakini alishindwa Januari, mwaka huu.

 

Kesi hiyo ilizua shutuma nyingi na hasira nchini China kutokana na matukio ya kikatili wanayokumbana nayo wanawake kwenye ndoa zao hivi sasa.

 Stori: Sifael Paul

Leave A Reply