The House of Favourite Newspapers

Apeshit Kama Hujaiona na Kuielewa Umechelewa Sana!

Beyoncé na Mumewe Jay Z, 

I CAN’T believe we made it,” Beyoncé kaimba maneno hayo kwenye wimbo mpya uitwao Apeshit, maneno yayomaanisha “Siamini kama tumefanikiwa.”

Maneno haya yana maana kubwa kwa Beyoncé, pengine kutokana na maajabu waliyofanya kwenye wimbo wao huo mpya. Hivi umeusikiliza? Vipi kichupa chake umekitazama? Kama hujasikia wala kukitazama kichupa basi umechelewa sana!

Apeshit, ni wimbo wa kwanza kwenye albamu iitwayo Everything Is Love, iliyoandaliwa na wanandoa Beyoncé na Jay Z, katika muunganiko wao waliouita The Carters kwa ajili ya kuandaa albamu hiyo.

NINI SPESHO KWENYE WIMBO HUU?

Ukiachana na mashairi yao, kitu spesho kwenye wimbo hu ni ubunifu kwenye kichupa chake walichokishutia kwenye jumba la makumbusho maarufu duniani liitwalo Louvre, ambalo lipo kule Paris, Ufaransa.

Pengine katika wimbo huo, kama ambavyo Beyoncé ameimba walitaka waonyeshe namna walivyofanikiwa kifedha na kimuziki kwamba wanaweza kufanya lolote lile wanalotaka kwenye muziki wao.

Ukweli ni kwamba ukitazama dola 17,500, ambazo ni zaidi ya bilioni 35 za Kibongo, walizotoa kwa siku moja kwa ajili ya kushuti video yao kwenye jumba hilo, si mchezo.

Mbali na gharama waliyotoa, kwenye video hiyo wawili hao wameonyesha juu ya utajiri wa michoro ya asili, tamaduni na sanamu zilizobuniwa na wabunifu maarufu duniani na kupewa heshima kubwa. Sanamu zenyewe ni hizi;

SANAMU YA WINGED VICTORY OF SAMOTHRACE

Hii ni sanamu ambayo inajulikana pia kwa jina la Nike of Samothrace. Ni sanamu ambayo ilichorwa karne ya pili na tangu mwaka 1884, ipo kwenye Jumba la Makumbusho la Lovre na ina maana ya mungu wa kike wa ushindi wa Kigiriki.

SANAMU YA VENUS DE MILO

Hii nayo ni sanamu ya Kigiriki ambayo inapamba kwenye jumba hilo la makumbusho na inadaiwa kutengenezwa kati ya mwaka 100 na 130. Inamaanisha mungu wa kike wa uzuri na upendo na ni kazi ya msanii Alexandros wa Antioch.

MCHORO WA MONA LISA

Kuna sehemu Beyoncé, anaonekana akiimba mbele ya mchoro uitwao Mona Lisa. Huu ni mchoro maarufu zaidi duniani, kuzungumziwa, kuandikwa na wanamuziki mbalimbali kuuimbia nyimbo. Mchoro huu ulichorwa na msanii kutoka Italia, ambaye pia ni mwa

ndishi wa vitabu aitwaye Leonardo da Vinci na unasadikiwa kwamba ni sura ya Lisa Gherardini, mke wa mfanyabiashara maarufu zamani Italia aitwaye Francesco del Giocondo. Sanamu hii ipo kwenye rekodi za duniani za Kitabu cha Guinness, baada ya mwaka 1962, kuingiza zaidi ya dola milioni 100 za Kimarekani ambazo ni zaidi ya bilioni 226 za Kibongo.

Sanamu ya Great Sphinx of Tanis

Sanamu hii ambayo inaonyesha mwili wa simba mwenye kichwa cha kiongozi wa zamani wa Misri aitwaye Pharaohs Amme

nemes II, ni miongoni mwa sanamu maarufu duniani ambazo zipo kwenye jumba hilo ambazo Beyoncé na Jay Z, walipenda kuzitumia kwenye video yao.

MCHORO WA NEGRESS

Mchoro huu wa mwanamke mweusi ambao ulichorwa karne ya 18 na msanii Marie- Guillemine Benoist, kipindi ambacho biashara ya watumwa ilikuwa inakomeshwa.

Mchoro huu umebaki kuwa alama ya kumbukumbu ya watu weusi katika taifa hilo na unaangaliwa kwa heshima ya tofauti hata pale tamaduni za Kiafrika zinapokuwa zinafukiwa kwenye taifa hilo.

KAVA LA ALBAMU YENYEWE

Kava la albamu hiyo ya Everything is Love, imechukuliwa kwenye ‘scene’ moja ya wimbo huo wa Apeshit, ambayo inawaonesha ‘dancers’ wawili kutoka kwenye video hiyo ambao ni Jasmine Harper na Nicholas ‘Slick’, wakiwa mbele ya mchoro wa Mona Lisa, huku Herper akionekana akimtengeneza nywele Slick.

Pozi hilo, linafananishwa na picha iliyowahi kupigwa mwanzoni mwa mwaka 1990 ikiwaonyesha watu wawili weusi Deana Lawson na Carrie Mae Weems, ambayo pia ni maarufu miongoni mwa picha zilizowahi kupigwa za watu weusi.

Ukiachana na haya yaliyo tajwa, ukweli ni kwamba kwenye video hii kuna mengi ya kufurahisha na kustaajabisha ambayo Beyoncé na Jay Z, wameyaonyesha pengine kuithibitishia dunia namna walivyofanikiwa na kwamba wanaweza kufanya chochote kile kwenye muziki wao

Makala: Boniphace Ngumije

Comments are closed.