The House of Favourite Newspapers

Kijana Shabani Nasoro Apigwa Ndoa Ya Mkeka Msibani

0

 

 Kijana Shabani Nassoro (kulia) mkazi wa Tuangoma jijini Dar akifungishwa ndoa msibani. 

WATU WEWEEEE! Julai 3, mwaka huu, kijana Shabani Nassoro mkazi wa Tuangoma jijini Dar amejikuta akipigwa ndoa ya mkeka kwenye msiba wa kaka wa mwanamke aitwaye Salma Zalmano aliyekuwa akiishi naye kienyeji.

Jamaa (katikati) akiwa amewekwa mtu kati huku mkewe akimuangalia.

ILIVYOKUWA Kwa mujibu wa chanzo chetu inadaiwa Nassoro alikuwa anaishi kinyumba na Salma kwa muda wa miaka mitatu bila kujitambulisha kwa ndugu zake wala kufunga ndoa kama ilivyo kwa jamii kubwa ya Kitanzania.

Mwanamke aitwaye Salma Zalmano.

 SALMA ATAFUTWA NA NDUGU BILA MAFANIKIO

Ndugu wa Salma walimtafuta sana ndugu yao kwa miaka mitatu bila mafanikio na wala hawakuwa wanajua kama ndugu yao anaishi kinyumba na Nassoro maeneo ya Tuangoma.

SALMA AIBULIWA NA MSIBA

Hivi karibuni Salma alifi wa na kaka yake, kwa kuwa msiba huwa unawakutanisha na kuwaibua ndugu ambao wanakuwa wakiishi mbalimbali, hatimaye Salma naye akawa ameibuliwa.

ATINGA NA HAWARA WAKE

Ilielezwa kuwa, msibani hapo Salma aliongozana na Nassoro, mtoto wao na mama mzazi wa Nassoro kwa ajili ya kuhudhuria msiba huo.

MAANDALIZI YA MSIBA YAFANYIKA

Maandalizi ya msiba yakafanyika kama kawaida, watu wakafanya taratibu zote kwa ajili ya kuusitiri mwili wa marehemu pasipo kujua kuwa ndugu walikuwa na maswali kwa Salma kutokana na kumuona akiwa ameongozana na Nassoro.

MAMA WA NASSORO ASEPA

Baada ya mazishi, mama wa Nassor aliondoka kimyakimya huku akiwaacha wengine wakimaliziamalizia msiba.

Wananchi wakiwa eneo la tukio.

MUDA WA KUJITAMBULISHA

Kama ilivyo kawaida ya misiba mingi ya Kiafrika, baada ya mazishi kuisha ukafi ka muda wa ndugu kujitambulisha na hapo ndipo Salma alipomtambulisha Nassoro kuwa ndiye mwanaume anayeishi naye kwa muda wote.

NDUGU WAHOJI NDOA

Ndugu walionekana kumfurahia shemeji yao huyo, kisha wakahoji kama wameshafunga ndoa. Salma alisema hawajafunga na mara kwa mara amekuwa akimtaka Nassoro wafanye hivyo lakini mwenza wake huyo amekuwa mgumu.

MWANAUME AWEKWA MTU KATI

Wanandugu waliposikia hivyo wakaamua kumuweka mtu kati jamaa huyo na kumwambia ni lazima wafunge ndoa halali ili waishi katika misingi ya dini na hapo ndipo taratibu zikaanza kufanyika fasta.

Jamaa katikati akiondoka na mkewe

Baada ya makubaliano hayo, safari ilianza kuelekea kwa shehe aliyekuwa mtaa wa pili ambapo walipofi ka huko, Nassoro aliazimwa kanzu na kofi a kisha kufungishwa ndoa ya fasta bila kuwepo kwa chai wala pilau na baadaye wawili hao wakaondoka eneo hilo kuelekea walikokuwa wakiishi wakiwa ni mke na mume.

MSEMAJI WA FAMILIA ATIA NENO

Akizungumza na Amani, mmoja wa wanandugu ambaye alifahamika kwa jina la Baba Fulu ‘Rasi wa Ukweli’ alisema amefurahishwa na kitendo cha dada yake kufunga ndoa. “Tulimtafuta sana mdogo wetu kwa muda mrefu lakini hatukumpata hadi hivi karibuni alivyofi ka msibani, ikabidi abanwe na ndugu zangu lakini nilivyomuelewesha kuhusu hiyo ya ndoa alinielewa na kukubali kumuoa,” alisema Baba Fulu. Kuona tukio zima la ndoa hii iliyowafurahisha wengi, tumekuwekea VIDEO HAPA CHINI.

STORI: MWANDISHI WETU, AMANI

Leave A Reply