The House of Favourite Newspapers

Ariana Grande, Pete Davidson Wasemekana Kuchumbiana

STAA wa muziki wa pop,  Ariana Grande na rafiki yake wa kiume mchekeshaji Pete Davidson, wamechumbiana baada ya wiki kadhaa za kukutana, linasema gazeti la People.

Wamarekani hao wawili wote wenye umri wa miaka 24 kila mmoja, walianza kukutana tangu mwezi Mei mwaka huu, mara tu Grande alipoachana na mpenzi wake wa zamani Mac Miller.

Davidson pia alithibitisha katikati ya Mwezi Mei pia kwamba alikuwa ameachana na rafiki yake wa kike wa muda mrefu, Cazzie David.

Kwa mujibu wa chanzo kilichofichua habari hiyo kwa gazeti la People, kuchumbiana huko kumefanyika hivi karibuni baina ya wapenzi hao waliopendana haraka katika muda mfupi.

 

Comments are closed.