The House of Favourite Newspapers

Askari wa Israel amuua kwa risasi msichana wa Kipalestina

0

Islaer with Palestina (2)Askari wa Israel akijitayarisha kumpiga risasi msichana mwenye asili ya Palestina, Hadeel al-Hashlamon.
Islaer with Palestina (4)..Askari wenzake wakimzuia asimfanye chochote binti huyo.Islaer with Palestina (5) Hofu ikitanda kwa maaskari hao.Islaer with Palestina (6)Hadeel al-Hashlamon akiwa chini baada ya kupigwa risasi.Islaer with Palestina (7)Maaskari hao wakimkagua Hadeel mara baada ya kumpiga risasi.Islaer with Palestina (1)Mwili wa marehemu Hadeel al-Hashlamon ukipelekwa hospitili kuhifadhiwa.Islaer with Palestina (3)

Mwanafamilia wa Hadeel al-Hashlamon akilia kwa uchungu mara baada kumpoteza nduguye.

Picha inaonyesha wakati ambapo askari wa Israel mwenye silaha akijitayarisha kumpiga risasi msichana wa Kipalestina (aliyevaa nikabu) sekunde chache baada ya msichana huyo kujaribu kumchoma kisu mlinzi wa Israel katika Ukingo wa Magharibi Magharibi.

Hadeel al-Hashlamon, mwenye umri wa miaka 18, alipigwa risasi jana katika Ukingo wa Magharibi baada ya kudorora kwa usalama katika eneo hilo kabla ya kuadhimishwa kwa sikukuu za Wayahudi na Waislam wiki hii.

Picha zilizochukuliwa muda mfupi kabla ya msichana huyo kuuawa zinaonyesha jinsi askari wasiopungua wawili wa Israel walivyokuwa wamemlenga na bunduki zao kabla ya kuuawa kwake.
Jeshi la Israel lilithibitisha mauaji hayo yaliyotokea katika mji wa Hebron ulio katika Ukingo wa Magharibi.

Msichana huyo aliyekuwa anasoma chuo kikuu, alikimbizwa katika hospitali moja nchini Israel akiwa mahututi ambapo baba yake, Salah al-Hashlamon, alisema baadaye kwamba alifariki kwa majeraha. Askari aliyemuua hakupata madhara yoyote.

NA DAILYMAILY

Leave A Reply