The House of Favourite Newspapers

AUNT AANIKA UHODARI WAKE KWENYE MAPENZI

Aunt Ezekiel

STAA wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel amesema kuwa ana sifa ya uhodari kwenye mapenzi na ndio maana akiingia sehemu huwa anaondoa wote waliokuwepo na kubaki yeye.  

 

Akizungumza na Risasi Jumamosi, Aunt alisema kuwa linapokuja suala l a kumpenda mtu hata akiwa na nani atamuachia tu kwani anajijua ni hodari wa kuondoa wote waliokuwa kwenye himaya hiyo.

 

“Siwezi kuanika moja kwa moja ninafanya nini na kwa nini wakiwa kwangu hawafurukuti, lakini najua wazi kuwa nina sifa hiyo na sijawahi kushindwa kwenye hilo,” alisema Aunt.

 

Aunt ambaye kwa sasa anapika na kupakua na Moze Iyobo, amepita kwa wanaume mbalimbali wakiwemo Hartmann Mbilinyi na Sunday Demonte ambao wote walikuwa wana watu wao lakini alipowanasa, aliwatuliza, wakawa hawafurukuti kwake.

STORI: Hamida Hassan, Dar

Comments are closed.