The House of Favourite Newspapers

AUNT AFUNGUKA KUDAIWA KODI YA PUB

Aunt Ezekiel

STAA wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel baada ya kudaiwa kukosa kodi ya kulipia pango la Pub yake iliyopo Kinondoni jijini Dar na kuifunga, mwenyewe amefungukia madai hayo na kueleza kilichotokea.  

 

Akizungumza na Risasi Jumamosi, Aunt alisema siyo kwamba amefunga Pub yake kwa sababu ya kudaiwa kodi bali eneo hilo anataka kufanya biashara nyingine na hiyo ya pub ataihamishia sehemu nyingine.

 

“Kwa nini nidaiwe kodi wakati nina biashara nyingine nafanya na zinaenda vizuri? Watu huongea vitu ambavyo hawavijui kabisa, nafanya marekebisho ili niweke biashara nyingine na hii nitaihamishia sehemu nyingine,” alisema Aunt.

TIMBWILI! Wakulima korosho nusura wazichape na viongozi!

Comments are closed.