The House of Favourite Newspapers

AUNT AZIJIBU ‘NYODO’ ZA WEMA

DAR ES SALAAM: UKIONA watu wamevaa nguo zinazofanana, basi ujue wameshona kitambaa kimoja, wengi huita saresare; Amani lina kionjo cha matukio ya kushabihiana kati ya Wema Sepetu na Aunt Ezekiel.

Wiki chache zilizopita muigizaji Aunt Ezekiel alishindwa kutokea kwenye sherehe ya kuzaliwa ya shosti yake Wema iliyofanyika jijini Dar es Salaam ambapo sababu za kuikacha sherehe hiyo zikidaiwa kuwa ni nguo aliyopanga kuvaa siku hiyo kuharibiwa na fundi. Wenye tatizo la usahaulifu waliichukulia poa tu sababu hiyo na hakukuwa na doti ya kuanzia mchoro lakini wapembua umbeya wakasema eti: “Kamlipizia ‘nyodo’ rafiki yake.”

KWA NINI KULIPIZA NYODO?

“Hakuna cha nguo kuharibiwa wala nini sema Aunt kaamua kumlipizia kisasi Wema kwa sababu naye hakuenda kwenye uzinduzi wa filamu yake iitwayo Mama,” aliandika mmoja wa wafuasi wa mtandao wa Instagram na kuungwa mkono na mashabiki wengi.

SABABU ZATAJWA

Sababu ya kuungwa mkono kwa hoja ya mdadisi huyo wa mitandaoni ni pale kisa cha Aunt kutofika kilipofanana kwa asilimia 99 na cha rafiki yake Wema alichokitoa wakati fulani aliposhindwa kuhudhuria sherehe ya uzinduzi wa viatu vya Idris Sultan ambaye ni mshindi wa Big Brother Africa 2014. “Wema hakwenda kwenye sherehe ya Idris alipoulizwa alisema fundi alimcheleweshea nguo.

“Kwenye uzinduzi wa filamu ya Aunt alifika kwa kuchelewa, kifupi Wema amekuwa mtu wa sababusababu nyingi za kutofika kwenye matukio ya wenzake,” aliandika kwenye mitandao ya kijamii msichana aliyejitambulisha kwa jina la MissMt. Aidha, kitu kingine kilichofanana na kile alichokifanya Wema kwa Aunt ni yeye kushiriki katika maandalizi yote lakini shughuli na kukwama kumalizia shughuli jambo ambalo Aunt naye alifanya vilevile.

Basi kufuatia waunganisha doti za mchoro wa umbeya kwenye jamii kupata pa kuanzia ndipo hali ya hewa mitandaoni ilipochafuka kwa watu kujaribu kuelezea hisia zao kuwa huenda Wema na Aunt wako kwenye bifu la chini kwa chini. Hapo ndipo Amani lilipoamua kuwatafuta mashosti hao wawili kwa lengo la ‘kupruvu’ kile kinachosemwa kwenye mitandao ya kijamii.

HEBU MSIKIE AUNT

“Sikuwa na sababu yoyote ya kunifanya nishindwe kufika kwenye sherehe ya Wema kwani nimeshirikiana naye hatua zote lakini kilichonikuta ndiyo hicho cha nguo na wala sijamlipizia chochote.

“Kwangu alichelewa tu na mwisho tulionana na picha alipiga, watu wanafananisha tukio la Idris ndiyo fundi alimharibia nguo Wema hakufanikiwa kufika,” alisema Aunt. Amani likaona huenda mwigizaji huyo anaficha mbawa kuogopa kupigwa ‘manati’ na Wema na hivyo kulazimika kuutafuta upande wa pili ili kujua nako hali ikoje.

WEMA AFUNGUKA

“Aunt aliniambia kuwa hatoweza kufika kwa kuwa amepata dharura lakini tulishirikiana katika kila kitu sasa anilipizie kisasi kwani mimi nina tatizo naye jamani!

Dharura ni kawaida kwa binadamu na nilimwelewa,” alisema Wema huku akionesha kupotezea kelele za mitandaoni ili mambo yasiwe mengi. Hata hivyo Wema na Aunt licha ya kuwa na urafiki wa karibu mara kadhaa urafiki wao umekuwa ukipanda na kushuka jambo ambalo katika hali ya kawaida ndiyo ubinadamu.

Stori: Shamuma Awadhi, Amani.

Comments are closed.