The House of Favourite Newspapers

AY Avimba Huko Youtube, Apokea Tuzo Maalum ya Mafanikio

0
AY Masta akiwa na Salama Jabir

AY; ni staa wa muziki wa Hip Hip Bongo ambaye sasa anavimba baada ya kupokea Silver Plaque (tuzo) kutoka Mtandao wa YouTube mara baada ya chaneli yake kufikisha subscribers (wafuasi) 100,000.

 

AY anayetamba na Ngoma ya Masta aliyomshirikisha Juma Nature anasema baada ya hatua hiyo kazi mpya inafuata hivi karibuni.

 

“Finally i got my YouTube Plaque, round hii hailali ni Kazi juu ya kazi, content juu ya content tufike wanafamilia 500,000 mpaka 1,000,000 na kuendelea. Kazi mpya soon so fanya ku-subscribe my channel AY Masta uwe wa kwanza kuona kazi zangu zijazo. One…” amesema AY.

AY akiwa na Rais Mstaafu wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete

Kwa kawaida YouTube wana tuzo sita ambazo hutoa kwa wazalishaji maudhui mbalimbali wakiwemo wasanii wa muziki na filamu kama ifuatavyo;

  1. Opal -Hutolewa kwa kufikisha subscribers 1,000.
  2. Bronze -Hutolewa kwa kufikisha subscribers 10,000.
  3. Silver Creator -Hutolewa kwa kufikisha subscribers 100,000.
  4. Gold Creator -Hutolewa kwa kufikisha subscribers 1,000,000 (milioni 1).
  5. Diamond Creator -Hutolewa kwa kufikisha subscribers 10,000,000 (milioni 10).
  6. Ruby Creator -Hutolewa kwa kufikisha subscribers 50,000,000 (milioni 50).

Cc; @sifaelpaul

Leave A Reply