The House of Favourite Newspapers

Baada ya Kimya cha Miaka 3, Rihanna Ametoa Kauli Hii

 

MWANAMUZIKI wa kike wa R&B na Pop, ‘Robyn Rihanna Fenty’,  maarufu kama Rihanna,  amefunguka kuachia albam yake ya ‘R9’ mwakani 2019 baada ya kuwa kimya kwa muda wa karibu miaka mitatu.

 

Siku ya ijumaa Desemba 21, mwaka huu,  katika mtandao wake wa Instagram alimjibu shabiki aliyemuuliza swali muda gani ataachia albam, akamjibu kwa kuandika, “2019”.

 

 

Kwa kipindi chote hicho mwanadada Riri alichokuwa kimya iliripotiwa alikuwa anashighulikia albam mbili.

 

Albam  ya rihanna ‘R9’ itakuwa ni ya tisa baada ya mafanikio makubwa ya ile ya ANTI ambayo aliiachia mwaka 2016 na ikafanikiwa kuingia namba moja kwenye albam bora 200 za Billboard.

 

Tarehe na mwezi wa kuachia albam yake bado havijajulikana.

Comments are closed.