BAADA YA KUSHINDA TUZO… CALISAH ATOA YA MOYONI

Calisah Abdulhamiid 

BAADA ya kufanikiwa kuiwakilisha vyema Tanzania na kuwa mshindi wa Mr Africa International 2018, huko nchini Nigeria mwanamitindo, Calisah Abdulhamiid ameelezea furaha aliyonayo kwa sasa kwa kuwashukuru Watanzania wote waliompigia kura na kuilalamikia Serikali kutompa sapoti katika safari yake ya kuelekea nchini humo.  

 

Calisah aliibuka mshindi wa Mr Africa huko nchini Nigeria Desemba 2. Akizungumza na Ijumaa Calisah alisema;

“Kwa kweli nilifarijika sana baada ya kutangazwa kuwa mimi ndio mshindi, licha ya kwamba kabla ya safari yangu ya kuelekea Nigeria nilipitia changamoto nyingi ikiwemo kutopata ushirikiano kabisa toka kwa Serikali yangu, kwa sababu hata bendera niliyoitumia niliishona mwenyewe kwa fundi, hivyo nimepata tabu sana mpaka kufikia hapa,” alisema Calisah.

NB: Usikose kusoma makala zaidi Magazeti Pendwa ya­nayofuatiwa.

Stori: Memorise Richard

Loading...

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment