BAADA YA NDINGA, MAUA: MASHABIKI WAMENIPA KIWANJA

Maua Sama

BAADA ya kufunga mwaka vizuri na Ngoma ya Iokote na kufanikiwa kuvuta ndinga aina ya Toyota RAV4, staa wa Bongo Fleva, Maua Sama amesema gari hilo lilitokana na sapoti ya mashabiki na kwamba kwa nguvu yao hiyohiyo amefanikiwa pia kununua kiwanja. 

 

 Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Maua alisema kuwa kwa sasa ameanza ujenzi wa ‘bangaloo hatari’ maeneo ya Mbweni jijini Dar.

 

“Mashabiki wangu ndiyo wamenipa mafanikio na kunifanya niweze kununua kitu ambacho nakitaka, hata hili gari limetoka kwao hakuna mtu mwingine zaidi ya mashabiki wangu na nipo mbioni kumalizia mjengo wangu kwa nguvu zao,” alisema Maua.

Loading...

Toa comment