The House of Favourite Newspapers

Baada ya Sukari… Sasa Hofu Dola Kufichwa Yatanda

0

Tanzania's President elect John Pombe Magufuli addresses members of the ruling Chama Cha Mapinduzi Party (CCM) at the party's sub-head office on Lumumba road in Dar es Salaam, October 30, 2015. Tanzania's ruling party candidate, John Magufuli, was declared winner on Thursday of a presidential election, after the national electoral body dismissed opposition complaints about the process and a demand for a recount. The election has been the most hotly contested race in the more than half a century of rule by the Chama Cha Mapinduzi Party, which fielded Magufuli, 56, a minister for public works. REUTERS/Sadi SaidRais John Pombe Magufuli.

DAR ES SALAAM: Baada ya baadhi ya wafanyabiashara kumhujumu Rais John Pombe Magufuli kwa kuficha sukari na hivyo kuifanya ipande bei, hofu kubwa imetanda juu ya kufichwa kwa fedha za kigeni ili zisiingie katika mzunguko na hivyo kusababisha mfumuko wa bei.

Habari kutoka chanzo ambacho ni mfanyabiashara anayesafirisha mazao nje (jina linahifadhiwa), alisema zipo dalili za kufichwa kwa dola ya Marekani inayotumika karibu dunia nzima, kwani katika baadhi ya maduka, fedha hizo haziuzwi, badala yake zinanunuliwa tu.

DOLLAR

“Juzi nilikuwa nataka kwenda shamba kidogo kuchukua mzigo, nikaenda pale Bereau de change (jina kapuni), nikabadilisha dola kupewa T shillings, lakini nikiwa njiani, nikapata udhuru ambao nilitakiwa nimtumie jamaa dola 2000 Dubai, nikamtuma wife aende pale dukani, akaambiwa dola hakuna wakati mimi nilibadili 4000 saa mbili tu nyuma,” kilisema chanzo hicho.

Mfanyabiashara huyo alisema, hakushangazwa sana na jambo hilo, lakini baada ya mkewe kukosa katika duka jingine, alianza kuhisi kama kuna mchezo mchafu unataka kuchezwa na wamiliki wa maduka hayo.

Sukari-001

Risasi Mchanganyiko lilifuatilia ishu hiyo kwa kutembelea maduka kadhaa yaliyoko Kinondoni na katikati ya jiji la Dar es Salaam ambako baadhi ya maduka yalionekana kubadilisha kwa kuuza aina nyingine za hela isipokuwa dola ya Marekani na pauni ya Uingereza.

Katika duka moja la Kinondoni, muuzaji mmoja aliyekataa kutaja jina lake, alisema suala la hujuma hadhani kama ni kweli, kwa sababu ukosefu na upatikanaji wa fedha za kigeni madukani ni jambo la kawaida.

“Ingawa kuna wakati huwa tunapewa maelekezo na wamiliki juu ya kiwango cha kuuza dola kwa siku, kikifikia hapo hatuendelei tena kuuza. Kama hili likifanywa ni hujuma, sisi hatuwezi kujua, labda kama ungewasiliana na mwenyewe,” alisema huku akikataa kutoa mawasiliano ya bosi wake.

Gazeti hili lilifanya juhudi za kumtafuta Zaria Mbeo ambaye ni Meneja Uhusiano wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ili azungumzie suala hilo, lakini hakupokea simu yake, bali alitumia ujumbe mfupi akisema yupo katika kikao, alichodai angemaliza saa 12 jioni.

Baada ya kujitambulisha na kutumiwa swali juu ya jambo hilo, Zaria hakujibu. Aidha, lilimtafuta pia Mkurugenzi wa Elimu kwa walipa kodi katika Mamlaka ya Mapato (TRA) ili kupata ufafanuzi wa madhara ya kutokuwepo kwa dola, lakini simu yake haikupatikana kutwa nzima juzi.

KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP

*********

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU:

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

ERIC SHIGONGO INSTAGRAM: @ericshigongo

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: GlobalPublishers

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE: @shigongotz

Leave A Reply