The House of Favourite Newspapers

BABA WA KANYE WEST AGUNDULIWA NA KANSA YA TEZI-DUME

Image result for kanye west and his father

Kanye akiwa na baba yake.

BABA wa mwanamuziki wa Marekani Kanye West aitwaye Ray West, anasumbuliwa na kansa ya tezi-dume na si ya tumbo kama ilivyoenezwa na vyombo vya habari.

Inasemekana Kanye ameacha shughuli zote ili kumshughulikia baba yake anayetibiwa huko Los Angeles na anaendelea vyema.

Ugonjwa huo umetokea baada ya zaidi ya miaka kumi ya kifo cha mama yake Kanye, marehemu Donda, mtu ambaye alikuwa kipenzi chake mkubwa  hadi kumsababishia kuchanganyikiwa mwaka 2016.

Ye (Kanye) alikuwa mtoto mdogo wakati baba yake na mama yake walipotengana, hata hivyo aliendelea kuwa na uhusiano mzuri na baba yake.

Comments are closed.