The House of Favourite Newspapers

Baba Atoa Mwaka Mmoja Msuva Kwenda Ulaya

BABA mzazi wa mwanasoka wa kulipwa, Simon Msuva anayekipiga katika Klabu ya Difaa Hassan El-Jadidi ya nchini Morocco, mzee Happygod Msuva amempa mwaka mmoja na nusu mchezaji huyo kwenda kucheza soka Ulaya.

Msuva alijiunga na Difaa akitokea Yanga katika msimu huu wa ligi kuu ya nchini Morocco huku akiwa mfungaji bora wa msimu uliopita katika Ligi Kuu Bara kwa kufunga mabao 14. Aidha katika muda mchache ambao Msuva ameichezea Difaa, amefanikiwa kufunga mabao 14 hadi sasa ambapo kati ya hayo, tisa ameyafunga katika mechi za kirafi ki na matano kati ya hayo amefunga kwenye ligi.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Mzee Msuva alisema, kabla mwanaye huyo hajaondoka nchini, alimsisitiza kutokaa Morocco zaidi ya misimu miwili na kumtaka akae mwaka mmoja na nusu kisha avuke mipaka ya kwenda kucheza soka la kulipwa katika timu za Ulaya.

“Alivyoondoka Msuva, nilimsihi asikae Morocco misimu miwili kwa maana ya kukaa miaka miwili ili aweze kwenda kucheza Bara la Ulaya kama vile Ufaransa, Hispania na Uingereza na hata akirejea hapa aweze kuitumikia timu yake ya taifa kwa nguvu zote hadi tone la mwisho.

 

“Kiwango chake kwa sasa kipo juu kwa jinsi nilivyoona clip zake anavyofunga anaonekana yupo vizuri sana na iwapo ataendelea hivi mara mbili au tatu nina uhakika atafi ka mabali sana. “Anachotakiwa hivi sasa ni kuendelea kudumisha nidhamu ambayo nilikuwa nikimsisitiza tangu nikiwa naishi naye na hilo sina wasi nalo, pia ni mtu mwenye uvumilivu,” alisema Mzee Msuva.

 

Khadija Mngwai, Dar es Salaam

Comments are closed.