The House of Favourite Newspapers

BABA WA ALIKIBA ALIVYOZIKWA MAKABURI YA KISUTU DAR (PICHA +VIDEO)

Mwili wa marehemu Saleh Kiba ukiombewa dua kabla ya kizikwa katika makaburi ya Kisutu jijini Dar jana.

BABA wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ally Kiba, marehemu Saleh Kiba ambaye alifariki juzi asubuhi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alizikwa  jana katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam. Mazishi hayo yalihudhuriwa na umati wa waombolezaji akiwemo Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamis Kigwangalah.

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ally Kiba (katikati, mwenye miwani) akiuombea dua mwili wa baba yake, marehemu Saleh Kiba.
Mwili ukitolewa msikitini kuelekea makaburi ya Kisutu. 
Safari ya kuelekea makaburuni  ikiendelea…

PICHA NA RICHARD BUKOS, GPL

Comments are closed.