The House of Favourite Newspapers

Babu Afunga Smartphone 11 Kwenye Baiskeli Ili Acheze ‘Game’

KIBABU, Chen San Yuan, wa Taiwan, amefunga simu 11 kwenye baiskeli yake ili kila aendapo aweze kucheza  michezo ya Pokemon iliyoko kwenye simu hizo.

Yuan, mwenye umri wa miaka 69 na anayeishi jiji la New Taipei, huzunguka na simu hizo kila mahali aendapo na akiingia mahali huzifungua kwenye baiskeli na kwenda nazo ili aweze kucheza wakati wowote.

h-54538639.jpg
Hulka hiyo ilianza mwaka 2016 wakati mjukuu wake alipomfundisha kucheza michezo hiyo ambayo imemjengea tabia hiyo  ya kuutumia muda wake asipokuwa kazini kucheza michezo hiyo.
h-54539265-1.jpg
Licha ya kwamba simu hizo zimemgharimu Paundi 1,165 (Sh. mil. 3.3), bado anataka kununua simu nyingine zaidi ili zifike 15.

Comments are closed.