The House of Favourite Newspapers

BABU WA MIAKA 73 ANASWA UBAKAJI WA BINTIYE

BABU mwenye umri wa miaka 73, aliyefahamika kwa jina la Nnko, mkazi wa Kikatiti Wilaya ya Arumeru mkoani hapa, amejikuta akiangua kilio hadharani baada kudakwa kwa ubakaji wa bintiye ambaye ni mtoto wa mdogo wake, Uwazi limedokezwa.  

 

Nnko alikamatwa wiki iliyopita akituhumiwa kwa ubakaji wa binti huyo ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi anayesoma darasa sita (jina lake na shule vinahifadhiwa), mwenye umri wa miaka 14.

Babu huyo alikamatwa kufuatia binti huyo kumtaja kuwa ndiye aliyembaka na kumpa ujauzito.Hata hivyo, kilio cha mzee huyo alichokitoa mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru (DC), Jerry Muro baada ya kukamatwa katika mkutano wa hadhara, hakikusaidia chochote kwani kiongozi huyo aliikomalia ishu hiyo na mzee huyo kujikuta akitiwa mbaroni na Jeshi la Polisi kisha kupelekwa mahabusu wakati ishu hiyo ikifanyiwa uchunguzi.

 

Akizungumza kwa uchungu, mama mzazi wa mwanafunzi huyo, Flora Nnko alisema mtuhumiwa ni shemeji yake na kwamba mwanaye alikuwa anakwenda kwake kama nyumbani kwao kwani ni binti yake kabisa kwa kuwa ni mtoto wa mdogo wake. “Ghafla tulishangaa kuona mtoto anaumwaumwa, mume wangu alipokwenda kumpima tukabaini ana ujauzito wa wiki nane.

 

“Tulipombana kwa kushirikiana na mwalimu wake ndipo akamtaja huyu shemeji yangu,” alisema Flora. Alisema kuwa, kitendo hicho kilimuuma mno kwa kuwa aliamini mtuhumiwa ni shemeji yake na pia ni sawa na baba wa mtoto huyo na kwamba ingemuwia vigumu kufanya kitendo kama hicho.

“Huyu mzee ni shemeji yangu, mke wake alishafariki dunia hivyo tunashirikiana katika masuala mbalimbali. “Nakumbuka Jumapili moja aliniomba mtoto akamsaidie kupukuchua mahindi, mimi nikaenda kanisani na niliporudi baadaye jioni mtoto alikuja na mahindi sadolini mbili,” alisema mama huyo.

 

Aliongeza kuwa, mara kadhaa alimruhusu binti yake kwenda kwa mzee Nnko kusaidia kazi ndogondogo kutokana na kwamba mzee huyo anaishi bila mke, mwanya ambao kwa mujibu wa mtoto huyo, aliutumia kumfanyia jambo hilo lisilofaa kwenye jamii. Alisema alimwacha mtoto wake amsaidie kazi mbalimbali za hapo nyumbani pale anapokuwa akimhitaji na alifanya hivyo akiamini kwamba busara za mzee huyo zingetumika kumwongoza mwanaye katika njia iliyo njema.

 

Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya ya Arumeru ambaye ni Mkuu wa Wilaya, Jerry Muro alisema ameamua kupambana kwa nguvu zote na tatizo la ubakaji katika wilaya yake. “Katika wilaya yetu tumeamua kutenga wiki nzima (iliyopita); tutapokea malalamiko ya wote waliobakwa na kupatiwa mimba kwa kipindi cha miaka mitano nyuma.Related image

“Hata kama kesi zao ziko mahakamani au Polisi waje kutueleza ili tuongeze nguvu zichukuliwe hatua za haraka,” alisema Muro. Alisema kuwa, matukio ya ubakaji na utiaji mimba kwa wasichana wenye umri mdogo yamekithiri wilayani humo na katika miaka miwili iliyopita, wanafunzi 84 wa shule za sekondari na msingi walikumbwa na tatizo hilo.

 

Alisema kutokana na vitendo hivyo kukithiri, Serikali wilayani humo imeamua kushirikiana na viongozi wa vyombo mbalimbali vya usalama kukabiliana na suala hilo kwa kuunda kamati maalum kwa ajili ya kushughulika na wahalifu na hakuna atakayepona.

 

Akizungumza mbele ya wanahabari, Mkuu wa Wilaya na Polisi, mzee Nnko alisema kwa huzuni kuwa yeye si mhusika wa mimba hiyo. Alisema tukio hilo la ubakaji na kumtia mimba mwanafunzi huyo limetengenezwa kwa lengo la kumharibia jina.

 

Naye Afisa Mtendaji wa Kata ya Kikatiti, Hamida Mnyenyelwa alisema alipata taarifa shuleni kwa mwanafunzi huyo kuhusu utoro wake na walianza kumfuatilia ndipo walipobaini ni mjamzito. “Tulipobaini tulimbana huyo mwanafunzi akamtaja huyu mzee Nnko kuhusika na anadaiwa alifanya naye tendo la ndoa mara mbili,” alisema mtendaji huyo wa kata.

BREAKING: JPM Apiga ‘STOP’ Sherehe Za Uhuru!

Comments are closed.