TECNO, miongoni mwa kampuni bora za simu ulimwenguni imezindua rasmi TECNO camon 11 ikiwa ni mwendelezo wa toleo la simu za TECNO camon. Simu za TECNO camon zimekuwa zenye ushawishi mkubwa sana kutokana na uwezo wa kamera na muonekano wake kwa ujumla, na katika uzinduzi huo TECNO ilitoa tamko rasmi kuhusiana na zoezi la ubadilishaji wa simu za camon kwa camon 11 mpya ikiwa imeambatana na ofa ya GB 15 kwa miezi mitatu bure kutoka Vodacom Plc.
Muonekano wa nje wa TECNO camon 11 unaofahamika kama ‘diamond fire design’ unaifanya camon 11 kuwa simu yenye kuvutia zaidi kati ya zote. Na japokuwa ni simu ya kwanza kuzalishwa na kampuni ya TECNO yenye teknolojia mpya katika kioo inayofahamika kama ‘notch’ lakini bado TECNO imehakikisha inaongeza mvuto katika simu hiyo kwa umbo jembamba lenye upana wa nchi 6.2HD+ na uwiano wa 19:9.
Zoezi zima la ubadilishaji wa simu za TECNO camon (camon cx, camon cx air, camon cm, camon x na x pro) linafanyika katika mikoa sita katika maduka ya TECNO yenye promosheni ambayo ni TECNO exclusive Bus Terminal, TECNO Triple B, TECNO Exclusive CCM Babati, Arusha shop, TECNO Exclusive China Plaza Smart Hub, TECNO Exclusive Mlimani City Smart Hub, TECNO Exclusive Samora Smart Hub, TECNO Exclusive Pablo Dodoma, TECNO Exclusive Mbeya Muna Shop, TECNO Exclusive Jambo, Mwanza Shop na TECNO Exclusive Tabora Shop.
Ofa hii ya ubadilishaji wa simu za camon kwa camon 11 litakuhitaji kufika kati ya maduka hapo juu ukiwa na simu ya TECNO camon na mshiko kidogo ili uweze kupatiwa camon 11 mpya na ofa ya GB 15 kuanzia sasa hadi tarehe 30 ya mwezi huu wa sikukuu za Christmas.
Kwa maelezo zaidi tafadhali tembelea kurasa zetu katika mitandao ya kijamii.
https://web.facebook.com/TECNOMobileTanzania/ https://www.instagram.com/tecnomobiletanzania/
Comments are closed.