
MOJA ya taarifa za wasanii wa Bongo Flevani, zinazo-trend mjini kwa sasa ni kuhusu mtafaruku uliopo kati Barnaba Classic na mkewe Mama Steve ambapo inadaiwa kuwa couple hiyo ipo kwenye ugomvi mkubwa na kwamba mpaka sasa wametengana kila mmoja akifanya mambo yake kivyake.
Kwenye uzinduzi wa Video ya SHUGA ya Mimi Mars ambaye ni mdogo wa Vee Money uliofanyika Club Next Door usiku wa kuamkia leo, Global TV Online imefanikiwa kumnasa Barnabaambaye ni mwandishi mahiri wa nyimbo za Bongo Fleva na mwimbaji kwenye tasnia hiyo, ambaye kwa mara ya kwanza hakusita kuufungukia ugomvi huo huku akianika kila kitu kilichotokea kati yake na mkewe huyo hadi kufikia hatua ya kuhitirafiana.
 Barnaba na mkewe sambamba na mtoto wao, Steve
Barnaba na mkewe sambamba na mtoto wao, Steve
Barnaba anafunguka hivi ===> Ni ngumu sana kujua kama mimi na mama watoto wangu tumegombana, kila mtu anazungumza la kwake kwa sababu hawajui kinachoendelea. Mimi na mama watoto wangu hatujagombana, tumepishana maneno tu!
Hakuna watu ambao hawakwazani, mimi na mamam watoto wangu hatujawahi  kugombana, tunapishana tu kauli. Hakuna mtu aliye mkamilifu, kila mtu anachangamoto zake na changamoto hizo ndo zinaweza kukuvusha kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Kikubwa naelewa nachokifanya basi mimi na-move on!

Barnaba (kushoto) akihojiwa na Shetta, kulia ni Mimi Mars
Kuhusu Maumivu anayoyapata baada ya mama watoto wake kuondoka.
Navyosikia naongelewa mtaani vizuri nafurahi. Hakuna mtu yeyote anapenda kuzungumzwa vibaya. Maumivu nayoyapata ni makubwa sanani sawa na maumivu unayosikiwa wewe ukijikata kidole. Alisema Barnaba
 
			

Comments are closed.