The House of Favourite Newspapers

BASATA Waja na Tukio Kubwa, Dr. Abbasi Asema si la Kukosa

0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr. Hassan Abbasi

BAADA ya kuanza na kampeni ya kukumbusha na kuhimiza utayari wa Watanzania juu ya kushiriki wa sensa ya watu na makazi mnamo tarehe 23 Agosti mwaka huu iliyojulikana kama SENSABIKA ambayo ilikuwa ikifanyika kwa njia ya mitandao, leo hii Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) limekuja na jambo jengine kubwa Zaidi.

 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr. Hassan Abbasi pamoja na BASATA leo hii wametangaza tukio kubwa la kimkakati linalolenga uhamasishaji wa watu juu ya suala zima la ushiriki wa wananchi kwenye sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika tarehe 23 ndani ya mwezi huu.

 

Tukio hilo lililopewa jina la “SENSUS BIGGEST EVENT” ambalo limepangwa kufanyika siku ya tarehe 21 mwezi huu katika viwanja vya Leaders linatarajiwa kuwakutanisha wadau wote wa BASATA pamoja na Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo.

 

Dr. Abbasi amesema kwamba kila aina ya sapraizi itakuwepo katika siku hiyo wakiwemo wasanii wakubwa watakao shiriki katika hafla hiyo pamoaja na maonesho mbalimbali ya Sanaa na utamaduni.

 

Pia, Dr. Abbasi amesema fursa itatolewa kwa wasanii mbalimbali kuonesha kazi zao zinazohusu uhamasishaji juu ya swala zima la sensa ya watu na makazi hivyo wawasilishe kazi zao BASATA ili ziweze kupitiwa na kupewa kibali ya kuonekana siku hiyo ya tukio.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa Dr. Mapana

Aidha Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa Dr. Mapana ameweka wazi kuwa maandalizi yote yamekamilika na uratibu wa vikundi na wasanii  waliopeleka kazi zao umekamilika na amesisitiza kuwa kazi zitakazochaguliwa kuoneshwa siku hiyo ni zile kazi zenye viwango vya hali ya juu, ili kutoa burudani ya uhakika wakati wakihamasisha watazamaji juu ya kushiriki sensa ya watu na makazi.

 

Viongozi wa mashirikisho ya sanaa pia walipata nafasi ya kuweka wazi mipango yao katika siku hiyo ya tukio hilo kubwa pamoja na muwakilishi wa Baraza la Michezo Tanzania aliyehakikisha ukamilifu wa maandalizi ya kimichezo kwenye tukio hilo.

Imeandikwa: Abdallah Ally kwa msaada wa mitandao.

 

 

Leave A Reply