The House of Favourite Newspapers
gunners X

BASATA Yamfungia Babu wa TikTok Miezi Sita na Faini Milioni Tatu

0
Seif Kassim Kisauji almaarufu ‘Babu wa TikTok’

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limemfungia Seif Kassim Kisauji almaarufu ‘Babu wa TikTok’ kutojihusisha na kazi za sanaa ndani na nje ya nchi kwa kipindi cha miezi sita kutokana na ukiukwaji wa maadili kama msanii aliyesajiliwa na BASATA.

Aidha ‘Babu wa TikTok’ ametozwa faini ya shilingi milioni 3 huku akitakiwa kulipa faini hiyo ndani ya siku saba kuanzia  Julai 22, 2024 baada ya BASATA kujiridhisha kuwa ametenda kosa la kimaadili wakati akitekeleza kazi zake za sanaa na limefikia maamuzi kumfungia kuanzia leo Julai 22, 2024.

Taarifa ya BASATA imebainisha kuwa limefikia uamuzi huo baada ya kumuita Kisauji kuhusiana na ukiukwaji wa maadili akiwa kama Msanii aliyesajiliwa na Baraza hilo kwa usajili Na. BST-9684-2023-2154 ambapo ukiukwani huo wa maadili ni kinyume na Kanuni ya 25 (6) ya Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa za mwaka 2018 na Mwongozo wa Uzingatiaji wa Maadili katika Kazi za Sanaa wa Mwaka 2023.

“Baraza la Sanaa la Taifa kupitia Sheria Na. 23 ya Mwaka 1984 na Maboresho yake ya Mwaka 2019 ina mamlaka ya kusimamia maadili ya msingi kwenye Sekta ya Sanaa kwa Kanuni ya 25(1)-(8) ya Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa za Mwaka 2018” imesema taarifa hiyo.

“Baraza limekwishatoa na kuzindua mwongozo wa maadili katika kazi za sanaa ambao unapatikana katika tovuti yetu basata.go.tz, hivyo ni jukumu la kila Msanii na Mdau wa Sanaa na jamii kuzingatia maadili katika kazi za sanaa”.

Leave A Reply