Bata la Lyyn Dubai usipime!

WAKATI watu wakidai kuwa hali ni ngumu, kwa upande wa mwanamuziki anayeanza kufanya vizuri kwenye Bongo Fleva, Irene Loiuse ‘Lyyn’ anakula zake bata nchini Dubai.  Akizungumza na Amani, Lyyn alisema kuwa kwenda kwake nchini Dubai, ni moja ya kujipongeza kwa kutimiza miaka kadhaa lakini kwa yeye kula bata kunamruhusu hivyo aachwe ajiachie kwenye mahoteli ya kifahari nchini humo.

“Mimi nashangaa sana mtu akila bata watu wataanza oooh kapelekwa na bwana jamani mimi najipenda sana na kula bata kama hizi ni kawaida yangu wala sio kitu kigeni kwangu,” alisema Lyyn huku akitupia picha mbalimbali mtandaoni zinazomuonesha akiponda raha jangwani nchini humo katika pikipiki za kukodi.

Stori: Imelda Mtema

Toa comment