The House of Favourite Newspapers

Bayern Kuwavaa PSG, Real Madrid Dhidi ya Liverpool Uefa

0

DROO  ya Robo Fainali ya ligi ya Mabingwa Ulaya (Uefa Champions League) ipangwa mchana wa leo Machi 19.

 

Ratiba hiyo inaonyesha   Manchester City ya England, itavaa Borussia Dortmund ya Ujerumani, wakati Fc Porto ya Ureno itacheza na matajiri wa London Chelsea.

 

Mabingwa watetezi wa kombe hilo Fc Bayern Munchen watapambana na Mabingwa ya Ufaransa Paris Saint Germain (PSG) na Real Madrid ya Uhispania watacheza dhidi ya Majogoo wa jiji la Anfield Liverpool.

 

Mechi za kwanza zitachezwa tarehe 6 na 7 mwezi Aprili, na marudiano wiki inayofuata yani tarehe 13 na 14 na mechi za Nusu fainali ni Aprili 27 na 28.

 

Leave A Reply